Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’.
STORI: Sifael Paul, Wikienda
Dar es Salaam: Hali ni mbaya! Vita ya ufisadi aliyoitangaza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ inadaiwa kuwalaza njaa wapiga dili mjini na madalali waliokuwa wamejazana kwenye taasisi za serikali.

Uchunguzi
wa gazeti hili kwenye taasisi kubwa zipatazo 20 zilizopo katika wizara
mbalimbali zenye makao yake makuu jijini Dar, umebaini kuwa, wale ‘watu
wa kati’ kwa sasa hawana dili kwani JPM ameziba mianya yote ya rushwa.
“Kama
alivyosema Ludovick Utouh (aliyekuwa Mkaguzi wa Hesabu za Serikali) kuwa
serikali na taasisi zake ilikuwa imejaa madalali na mafisadi ni ukweli
mtupu.
“Ilikuwa
ni vigumu kupatiwa huduma bila kujuana au kuwepo kwa mtu wa kati
aliyekuwa pale kwa ajili ya kukamilisha dili, lakini sasa wanapiga tu
miayo mitaani. Kweli JPM amenyoosha watu,” alisema mmoja wa wananchi
waliojitokeza kupata huduma kwenye Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya
Makazi na kudakiwa na mwingine:
“Kwenye mashirika ya umma hali ilikuwa mbaya mno.
“Kwenye mashirika ya umma hali ilikuwa mbaya mno.
Ndiyo
maana tunasema JPM aachwe akomeshe watu kwa sababu ameachiwa nchi
iliyooza, yenye sera mbovu za kukumbatia na kuruhusu wapiga dili
kuliibia taifa.”
Miezi kadhaa baada ya kuishika nchi, Rais Magufuli alikuwa na kazi kubwa ya kupanga mikakati ya kuijenga Tanzania mpya kwa kupiga vita ufisadi hivyo hata kama kuna wachache wanaolala njaa kwa mkakati wake huo ni heri walale njaa lakini Watanzania walio wengi wapate neema.

0 maoni:
Chapisha Maoni