Rais wa
Brazil, Dilma Rousseff amehaidi kupambana mpaka mwisho na jitihada
zinazompinga ili kutetea demokrasia ya Brazil.Mwishoni mwa juma
lililopita baraza la seneti liliweza kuhalalisha tuhuma hizo kwa kupiga
kura ya kutokuwa na Imani na Rais Rousseff ambaye ameshutumiwa kwa
kufanya mabadiliko katika bajeti ya fedha jambo ambalo lilishutumiwa
vikali.
Katika
hatua yake ya kwanza ambayo raisi huyo kufanya baada ya kura kupigwa
,amesema dhamira yake ilikua safi na hajafanya jambo lolote kinyume cha
sheria.
Baraza la
seneti linatarajia kufungua mashitaka ya mtu kupigiwa kura ya kutiliwa
shaka ifikapo mwezi ujao na kumfanya rais kusimamishwa katika wadhifa
wake kwa muda wakati kesi ikiendelea.
Lakini
Rais Rousseff alisema hana mpango wa kuachia wadhifa wake huo na kusema
"nitaendeleza mapambano haya kwa kupitia taratibu zote,kuanzia hiyo
iliyowekwa na baraza la seneti kwa kuwa nina uhakika nitaweza kupata
fursa ya kujitetea."
|
0 maoni:
Chapisha Maoni