Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( wa pili kulia) akifurahia jambo na
Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson (kulia) wakati wa KUFUNGA Tamasha la
Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe
mkoani Mbeya leo Oktoba 08,2016.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( katikati) akicheza moja ya ngoma za
kiutamaduni Wwakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition
Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo Oktoba
08,2016 kulia ni Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson na kushoto ni Katibu
Mtendaji BASATA Geodfrey Mngereza.
Kikundi cha Utamaduni cha Ikama
kikitoa burudani wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia
Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo
Oktoba 08,2016.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM.
…………………………………………………………
Na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM -Mbeya
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewashauri vijana kutumia ngoma za
asili kujiajiri kwani ni fursa mojawapo ya ajira kwa sasa.
Ametoa ushauri huo leo Mjini
Mbeya alipokuwa akifunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition
Festival 2016 na kuwahimiza vijana kutosubiri kuajiriwa ikiwa wanaona
wana uwezo wa kufanya kitu ambacho kitawasaidia kupata kipato na
kuendesha maisha yao.
“Ngoma za asili ni chanzo cha
ajira kwa vijana na sisi kama Serikali tutashirikiana na wadau wa Sanaa
na Utamaduni ili kutengeneza ajira na kudumisha mila na desturi za nchi
yetu” alisistiza Mhe. Nnauye.
Aidha kwa upande wake Naibu Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson amesema
kuwa fursa pekee kwa vijana kujiajiri kupitia shughuli za Sanaa na
Utamaduni kwani ndio sekta ambazo zimetoa ajira kwa vijana wengi duniani
kwa sasa.
“Nawashauri vijana wa kitanzania
kuangalia na upande huu wa Sanaa na Utamaduni kuna ajira pia na sisi
tupo pamoja nao na tutawapa ushirikiano ili wafikie malengo” alisema
Mhe. Tulia.
Tamasha hili liliondaliwa na
Naibu Spika Mhe.Tulia Ackson linafanyika kwa siku mbili na
limeshirikisha vikundi vya ngoma za asili vipatavyo 62 kutoka mikoa
mbalimbali nchini.
0 maoni:
Chapisha Maoni