NA VICTOR MASANGU, MKURANGA
CHAMA
cha soka Mkoa wa Pwani (COREFA) kimepata safu mpya ya uongozi
wataoongoza kwa kipindi cha miaka minne ambapo katika nafasi ya
mwenyekiti imekwenda kwa Hassan Hasanoo baada ya kuchaguliwa kwa
kishindo na wajumbe wa mkutano mkuu uliofanyika katika ukumbi wa kiguza
Wilayani Mkuranga.
Katika
uchaguzi huo ambao ulikuwa unasubiliwa kwa hamu na shauku kubwa na
wadau wa mchezo wa soka ulihudhuriwa na viongozi wa serikali,viongozi
wa michezo kutoka wilaya mbali mbali za Mkoa wa Pwani, waangalizi kutoka
shirikisho la soka Tanzania (TFF) wakiongozwa na mkurugenzi wa sheria
na wanachama Eliud Mvella.
Hassanoo
ambaye hapo awali alikuwa katika nafasi hiyo ya mwenyekiti ameweza
kutetetea kiti hicho kutokana na kuwa mgombea pekee aliyowania nafasi
hiyo baada ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi kumpigia kura za
ndiyo zipatazo 22 katika ya kura 24 zilizopigwa huku akipigiwa kura mbii
za hapana.
Akitangaza
matokeo hayo Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa Chama cha soka Mkoa wa
Pwani (COREFA) Masau Bwire alisema kuwa nafasi ya Mwenyekiti
imenyakuliwa na Hassan Hasanoo aliyepata kura 22 za ndiyo, huku nafasi
ya makamu mwenyekiti ikichukuliwa na Shabani Kangale(Macho kodo) kutoka
Wilayani Bagamoyo kwa kujipatia kura 14 dhidi ya mpinzani wake Said
Baiza alipata kura tisa.
Kinyang’anyiro
kingine katika uchaguzi huo kilikuwa katika nafasi ya katibu mkuu,
ambapo kulikuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na wagombea wote
watatu waliokuwa wanaomba kura kuonekana kila mmoja kuwa na dalili za
kuondoka na ushindi hivyo kuonekana muda wote wakiwa wana haha uku na
kule.
Uchaguzi
wa nafasi hiyo ya ukatibu mkuu ilibidi urudiwe kwa mara ya pili
kutokana na wagombea wawili kupata kura sawa,ambapo Robert Mnisi
alipata kura (8) Abubakari alawi kura (8) huku aliyewahi kuwa katibu
mkuu wa zamani COREFA Riziki Majala akipata kura 7, hivyo ikamlazimu
Mwenyekiti wa uchaguzi kutangaza kurudia upya katika nafasi hizo mbili.
Baada
ya uchaguzi huo kurudiwa tena kwa mara nyingine , matokeo yaliweza
kubadilika na kuacha midomo ya watu wazi kutokana na mwenendo mzima
ulivyokuwa, ambapo Abubakari Alawi aliweza kupata kura 16 na kutangazwa
rasmi kuwa katika mkuu, huku mpinzani wake wa awali Robert Mnisi
akipata kura 6 tu huku nafasi ya katibu msaidizi ikienda kwa Godfrey
Haule kwa kupata kura 17 za ndiyo.
Katika
nafasi ya Mweka hazina alichaguliwa Bernad Yomba Yomba kwa kupata kura
19 za ndiyo, wakati nafasi ya msaidizi wake ikinyakuliwa na Mohamed
Lubondo aliyejizolea kura 21 za ndiyo,kutoka kwa wajumbe wa mkutano
mkuu wa uchaguzi huo.
Makamu
wa Rais wa klabu ya soka ya Simba Jofrey Nyange (Kaburu) aliweza
kuitetea nafasi yake ya mwakilishi wa mkutano mkuu wa TFF, baada ya
kuweza kupata kura 21 za ndiyo, ambapo Juma Kisomo kutoka visiwani mafia
aliweza kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa klabu Mkoa baada ya kupata kura
zote 24 za ndiyo.
Kwa
wa nafasi za wajumbe wa kamati ya utendaji ya COREFA,zilinyakuliwa na
Mohamed Mbaruku kura (21) Shaban Mawingu (22) pamoja na mwamuzi mstaafu
wa ligi kuu ya Tanzania bara Saimon Mberwa aliyepata kura zote 24,huku
nafasi maalumu ya mjumbe katika soka la wanawake ikinyakuliwa na
Frorence Ambonisye kwa kupigiwa kura 23 za ndiyo.
Mwenyekiti
mpya wa Corefa Hassan Hassonoo (mpiganaji) mara baada ya kutangazwa
mshindi alitoa pongezi kwa wajumbe wa mkutano mkuu kwa kumchagua tena na
kuwahakikishia kwamba atashirikiana nao bega kwa bega katika kuleta
mabadiliko chanya katika kukuza mchezo wa soka katika Mkoa wa Pwani
kuanzia ngazi za chini kwa kuanzisha ligi za vijana wadogo .
Mara
baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo mkuu Mwenyekiti wa kamati ya
uchaguzi ya Corefa Masau Bwire aliweza kutumia fursa katika mkutano huo
kutangaza rasmi kustaafu na kuachia nafasi hiyo kutokana na kuchukizwa
na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimfanyika fitina , chuki na vitisho
katika kutimiza wajibu wake kulingana na kufuata kanuni, sheria na
taratibu zilizowekwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni