Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba(katikati), akizungumza na watendaji wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), Bi.
Kaitlin Meredi (kulia) na Johan Kruger(kushoto), walipomtembelea
ofisini kwake,jijini Dar es Salaam,leo. Ziara hiyo ikiwa na lengo la
kujadili njia muafaka za kukabiliana na biashara, matumizi na athari za
dawa za kulevya kwa jamii.
Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na
Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa
la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC),Johan Kruger(kushoto),
akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba
(katikati),walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuzungumzia juhudi
mbalimbali za kupambana na biashara haramu ya Dawa za Kulevya.Kulia ni
Mratibu wa Kupambana na Uhalifu wa Majini, Kaitlin Meredith.
Mratibu wa Programu ya Kupambana
na Uhalifu wa Majini kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na
Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), Kaitlin Meredith (kulia),
akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba,
masuala yanayohusu udhibiti wa uhalifu unaofanyika majini
walipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba (katikati),akiagana na Mratibu wa Programu ya
Kupambana na Uhalifu wa Majini, Kaitlin Meredith, mara baada ya
kumaliza mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa waziri, jijini Dar es
Salaam, leo.Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Biashara Haramu ya
Dawa za Kulevya kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na
Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), Johan Kruger (Picha Zote na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi)
0 maoni:
Chapisha Maoni