Postedy by Esta Malibiche on August 3.2016 in News
Zoezi la uchangiaji Damu likiendelea katika makao makuu ya TAZARA ambapo wafanyakazi mbalimbali wa Shirika hilo na watanzania wengine wamejitokeza kucnagia damu |
Wakati
Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia TAZARA wakiadhimisha miaka 40 ya
uwepo wake nchini Tanzania maadhimisho hayo yameenda sambamba na zoezi
maalum la kuchangia damu zoezi ambalo limefanyika makao makuu ya TAZARA
Dar es salaam Tanzania ambapo wafanyakazi wake wameitumia siku ya leo
kuchangia damu zoezi ambalo liliongozwa na mpango wa Taifa wa damu
salama Tanzania.
Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG BRUNO TANDU CHINGANDU akizngumza na wanahabari wakati wakiendelea na zoezi la ucnagiaji wa Damu |
Akizungumza
na wanahabari wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi mtendaji wa Tazara ENG
BRUNO TANDU CHINGANDU amesema kutokana na uhitaji mkubwa wa Damu uliopo
Tanzania wao kama TAZARA wameamua kusitisha shughuli za leo kwa ajili ya
kufanya zoezi moja la kuchagia damu zoezi ambalo linaenda sambamba na
maadhimisho ya miaka 40 ya kuanzishwa kwake.
Aidha
mmoja kati ya wahamashishaji kutoka mpango wa taifa wa Damu salama
Tanzania Bi Mariam Juma amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhitaji mkubwa
damu kutokana na kuongezeka kwa maswala mbalimbali yakiwemo ya
ajali,vifo vya mama na watoto wakati wa kujifungua wanaofariki kwa
kukosa damu,na magonjwa mengine mengi hivyo akawataka watanzania
kujitahidi na kuhakikisha kuwa angalau wanachangia damu kwa mwaka japo
mara mbili ili kuokoa maisha ya watanzania wenzao.
Mmoja kati ya wahamashishaji kutoka mpango wa Taifa wa Damu salama Tanzania Bi Mariam Juma akifafanua jambo juu ya umuhimu wa kucnagia Damu kwa watanzania. |
0 maoni:
Chapisha Maoni