Mkuu
wa Mkoa wa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe (Kushoto) akisalimiana
na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa ufunguzi wa
maonyesho ya Nane Nane katika uwanja wa maonyesho ya kilimo Nzuguni
Mkoani Dod
Viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Singida wakitembelea baadhi ya vibanda vya maonyesho wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Nane Nane
Baadhi
ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Singida wakiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe wakikagua eneo la maonyesho ya
kilimo cha zao la zabibu
Baadhi
ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Singida wakiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe wakikagua eneo la maonyesho ya mboga
mboga
Baadhi
ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Singida wakiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe wakikagua eneo la maonyesho ya bwawa
la samaki lenye samaki aina ya perege, kambare na kamongo liloandaliwa
na Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba
………………………………………………………………………………………………………
Na Mathias Canal, Dodoma
Ufunguzi wa siku kuu ya wakulima
Nane nane Kanda ya kati Dodoma mwaka 2016 umefanyika leo katika Uwanja
wa Maonyesho ya kilimo Nzuguni Mkoani Dodoma huku kauli mbiu ya mwaka
huu ikiwa ni “Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ni nguzo ya maendeleo, Kijana
shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).
Maonyesho haya yanahusisha
shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi,
wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo,
wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, taasisi za
umma na za binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akizungumza katika ufunguzi huo
Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe
amesema kuwa sekta ya kilimo bado ni mhimili wa uchumi wa Tanzania kwa
sababu inaajiri zaidi ya asilimia takribani 80 ya watanzania na kwa
kuzingatia malengo ya maendeleo ya Taifa ya kuwa nchi yenye uchumi wa
kati unaotegemea viwanda hivyo kilimo kikiboreshwa viwanda vitapata
malighafi ya uhakika na kuimarisha masoko kwa wakulima hivyo kuwepo na
ajira ya kuaminika kwa vijana na watanzania kwa ujumla.
Rc Mtigumwe amesema kuwa wastani
wa ukuaji wa sekta ya kilimo unabadilika mwaka hadi mwaka kutokana na
kilimo kwa kiwango kikubwa kutegemea mvua ambazo zimekuwa zikinyesha kwa
viwango na mtawanyiko unaotofautiana kila mwaka ambapo kwa mwaka 2010
sekta ya kilimo ilikuwa kwa asilimia 4 ikilinganishwa na asilimia 6.5 ya
mwaka 2015.
“Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali
zinaonyesha kuwa kanda ya kati ina rasilimali ya maji yakutosha ya chini
ya ardhi hivyo kuendelea kuitamka kama kanda kame hakuna usahihi wa
jambo hilo ipo haja ya kuona kuwa rasilimali hiyo inapatikana kwa ajili
ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji hivyo kupunguza kilimo cha
kutegemea mvua” Alisema Mtigumwe
Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida
kabla ya kuwahutubia wananchi waliojitokeza katika ufunguzi huo
alitembelea baadhi ya mabanda ya maonesho na kuona shughuli mbalimbali
za uzalishaji wa mazao, ufugaji, uvuvi, usindikaji na wauzaji wa zana na
pembejeo za kilimo ambapo amejionea matokeo ya juhudi mbalimbali
zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kuinua ukuaji wa sekta
ya kilimo ambapo juhudi hizo zinajumuisha uzalishaji wa mbegu mbalimbali
zinazostahimili hali ya hewa ya maeneo ya kanda ya kati.
“Natoa wito maalumu kwa wakulima,
wafugaji, wavuvi, wajasiriamali na wadau wa sekta zingine kuhakikisha
kuwa bidhaa zenu zinafikia ubora wa hali ya juu kuanzia shambani
zinakozalishwa, zinakosindikwa na kuhifadhiwa na hadi kumfikia mlaji,
ikumbukwe kwamba kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu
kutawezesha bidhaa zetu kuhimili ushindani wa hapa nchini na nje ya nchi
na kuuzwa kwa bei nzuri” Alisema Mtigumwe
Akitoa neno la shukrani kwa niaba
ya waandaaji wa maonyesho ya Kilimo, Mifugo na sherehe za nane nane,
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Miraji Jumanne Mtaturu amesema
kuwa hotuba ya Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida itakuwa ya
mazingatio ili kurahisisha na kuendeleza kasi ya serikali ya awamu ya
Tano kwa vitendo hususani katika kuakisi na kuwasaidia wananchi ambao ni
wakulima na wafugaji kupata mbinu bora za kufuga na kulima kisasa ili
kupata mazao kwa wingi.
Hata hivyo Dc Mtaturu amesema
kuwa ana imani thabiti kuwa baada ya kumalizika kwa maonyesho hayo
wakulima, wafugaji na wananchi washiriki watakuwa wamejifunza vyema
mbinu bora za kukabiliana na changamoto za kilimo na ufugaji hivyo
kujikita zaidi katika mbinu bora na za kisasa za kilimo na ufugaji pia.
Dc Mtaturu amesema kuwa shughuli
kuu ya wakazi wa kanda ya kati inayoundwa na mikoa miwili ya Singida na
Dodoma yenye jumla ya Wilaya kumi na mbili na Halmashauri 15 shughuli
zao kuu ni kilimo na ufugaji.
0 maoni:
Chapisha Maoni