Ndoto ya mashabiki wa Arsenal kuona sura mpya katika kikosi chao kufuatia kupoteza mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Liverpool, inaonekana kuanza kuonekana kama itakuwa tayari kuipata saini ya mshambuliaji wa Lyon, Alexandre Lacazette.
Hilo limejulikana baada ya Lacazette kufunguka kuwa atakuwa tayari kujiunga na klabu nyingine iwapo tu itafikia makubaliano na timu yake anayoitumikia sasa ya Lyon ya Ufaransa.
“Kama kutakuwa na ofa ambayo haitakataliwa, na mimi sitakataa,” alisema Lacazette wakati akifanya mahojiano na kituo cha tv cha Ufaransa na kuongeza.
“Lakini najisikia vizuri kuwa Lyon, usahihi ni kuwa maamuzi ninayoyafanya yanatoka katika akili yangu”