Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Dk. Hamisi Kigwangalla muda huu amefanya ziara ya kushtukiza katika Taasisi ya kijamii inayojishughulisha na masuala ya kutoa elimu kwa vijana na mapambano dhidi ya UKIMWI  ijulikanayo kama “The Community Health Education Services & Advocacy” (CHESA)  yenye maskani yake Upanga  Jijijni Dar e Salaam.
Naibu Waziri wa Afya amebainisha kuwa, amefanya ziara hiyo ya kushtukiza kutokana na taarifa za kiinterejensia juu ya kuwapo kwa vituo vingi vinavyojihusisha na masuala ya mapenzi ya jinsia moja ambapo taarifa za duru za kiusalama zikielezea kuwa kituo hicho cha CHESA kuchochea masuala hayo ambayo hapa nchini ni kinyume na sheria.