Diwani wa Kata ya Kibamba Ernest
Mgawe akizungumza na baadhi ya wananchi wa mtaa wa hondogo baada ya
nyumba zao walizokuwa wakiishi kubomolewa bila ya kufuata utaratibu wa
kisheria na kusababisha watu zaidi ya 30 kukosa makazi ya kuishi (Picha
na Victor Masangu)
Diwani wa Kata ya Kibamba Ernest
Mgawe akiwaonyesha wananchi wa mtaa wa hondogo barua iliyoandikwa kutoka
kwa Kamishina wa ardhi kuhusiana na kushughulikia taratibu zote kwa
ajili ya viwanja na sio kubomoa.(Picha na Victor Masangu)
Baadhi ya wakazi wa eneo hio la
mtaa wa hondogo wamekiwa wameketi chini wakijadiliana jambo baada ya
nyumba zao kubomolewa bila ya kuzingatia sheria na taratibu kwa madai
walivamia eneo ambalo lilikuwa linammiiki wake wakati eneo hilo
wameinunua kihalali.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo la
mtaa wa hondogo kata ya Kibamba akielezea kwa uchungu kwa waandishi wa
habari waliofika katika eneo hili kushuhudia baadhi ya nyumba
zilizobomolewa bila ya kufuata utaratibu wowote wa kiserikali.(Picha na
Victor Masangu)
…………………………………………………………………………………………….
NA VICTOR MASANGU, KIBAMBA
WAKAZI zaidi ya 30 wanaoishi
katika mtaa wa Hondogo kata ya Kibamba Wilayani Kiondoni Jijini Dar es
Salaam wamejikuta hawana makazi ya kuishi kutokana na nyumba zao
kubomolewa bila ya kuzingatia sheria na taratibu kinyume kabisa na haki
za binadamu.
Kubomolewa kwa nyumba hizo
kumepelekea kwa sasa wananchi hao kuishi katika hali ya sintofahamu
kwani nyumba zao walizokuwa wanazitegemea na familia zao zimevunjwa
hivyo baadhi yao wameamua kujihifadhi kwa muda kwa majirani zao kutokana
na kukubwa na hali hiyo.
Wakizungumza kwa uchungu na
katika eneo hilo wakazi hao akiwemo Miriam Mbeleselwa, Ramadhani
Kimaro,pamoja na Daima Kimaro walisema kwamba kitendo walichofanyiwa
ni cha kinyma na ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwani wamevunjiwa
nyumba zao bila ya kupewa taarifa yoyote na wamepata hasara kutokana na
mali zao nyingi zilizokuwemo ndani kuharibiwa vibaya.
Aidha wananchi hao walisema
wamesikitishwa na kitendo kilichofanywa na jeshi la polisi kusimamia
zoezi hilo la kuvunja nyumba lifanyike licha ya wananchi hao kuwaonyesha
nakala ya hati ya hukumu kutoka mahakama kuu ya adrhi lakini wao
walikaidi hukumu ya mahakama na kuamuru kuendelea kuwabomolea wananchi
hao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
serikali ya mtaa wa hondogo Juliasi Sulena alisema kuwa sakata hilo la
mgogoro kwa wananchi wa mataa wake analitambua vizuri na kuwa
lilishafika katika vyombo husika na limeshafanyiwa kazi na kuongeza kuwa
mahaka kuu ya ardhi ilishataoa hukumu kuwa wananchi hao wameshinda
kesi.
Nae Diwani wa kata ya Kibamba
Ernest Mgawe ambaye alifika kushuhudia athari walizozipata wananchi wa
mtaa wa hondongo baada ya kuvunjiwa nyumba ameitaka serikali kuwachukuia
hatua kali za kisheria watu wote waliohusika katika kubomoa nyumba
hizo.
Mgawe alisema kwamba wananchi
hao wa mtaa wa hondogo wameonewa kwani hawakupatiwa taarifa yoyote juu
ya kubomolewa nyumba zao , hivyo ameahidi kushirikina nao bega kwa bega
katika kipindi hiki kigumu ili aweze kuona ni namna gani anaweza
kuwasaidia .
KUBOMOLEWA kwa nyumba hizo tano
katika mtaa wa hondogo kata ya Kibamba Wilayani Kinondoni kumepelekea
zaidi ya watu 30 kukosa makazi ya kuishi kutokana na mgogoro huo wa
kugombania ardhi ambayo hukumu yake tayari ilishatolewa na mahakama kuwa
wananchi hao wameshinda kesi hiyo kihalali.






0 maoni:
Chapisha Maoni