Jumatatu, 4 Aprili 2016

TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
NEMBO YA TAIFATAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 4 APRILI, 2016
Ndugu wanahabari,
Kila wiki serikali kupitia Wizara yangu imekuwa ikitoa taarifa ya mwenendo wa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu na hatua zinazochukuliwa kudhibiti ugonjwa huu. Aidha pia kila mwisho wa mwezi, majumusiho hufanyika na kutolewa taarifa. Hadi kufikia tarehe 4 April 2016, jumla ya wagonjwa 20,294 wametolewa taarifa, na kati ya hao 320 wamepoteza maisha
Kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka, mwenendo wa Kipindupindu unaashiria kuwa idadi ya wagonjwa inaongezeka nchini. Mwezi Januari kulikuwa na wagonjwa 2,272, na mwezi Machi kulikuwa na wagonjwa 2,956. Hili ni ongezeko la asilimia 30.1%. Hata hivyo, baadhi ya mikoa imeonyesha uendelevu wa kupungua kwa idadi ya wagojwa wa Kipindupindu kwa robo ya kwanza. Mikoa hiyo ni pamoja na Simiyu, Rukwa na Mbeya. Takwimu hizi za nchi nzima zinaashiria kuwa juhudi za kupambana na ugonjwa wa Kipindupindu zinahitaji
kutekelezwa na kusimamiwa kikamilifu na mikoa na wilaya zote nchini baada ya Wizara yangu kutoa maelekezo na miongozo stahili. Vile vile, napenda kusisitiza kwamba hata Mikoa ambayo haina wagonjwa ni lazima wachukue hatua za tahadhari kuzuia maambukizi mapya, na ile mikoa ambayo ina wagonjwa iendelee kusimamia kikamilifu udhibiti wa mlipuko.
Katika mwezi Machi, jumla ya wagonjwa wapya walioripotiwa nchi nzima walikuwa 2,956, na vifo vilikuwa 53. Takwimu za mwezi Machi (tarehe 5 Machi hadi 3 Aprili) zinaonyesha idadi ya wagonjwa imeongezeka kwa asililmia 59.5% ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa wa mwezi Februari (1,853). Mikoa ya Tanga, Pwani na Mtwara haikuwa imeriporti wagonjwa mwezi wa Februari lakini mwezi huu wa Machi imepata wagonjwa wapya. Aidha katika kipindi hiki cha mwezi mmoja kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wapya kwenye mikoa ya Geita, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, na Dodoma. Idadi ya wagonjwa kutoka mikoa ya Simiyu, Mbeya na Iringa imepungua kati ya Februari na Machi 2016.
Kwa upande wa takwimu za kila wiki (weekly report), idadi ya wagonjwa wa Kipindupindu walioripotiwa kwa wiki ya kati ya tarehe 28 Machi hadi 3 Aprili 2016 imepungua kwa asilimia 37.2 ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa walioripotiwa kati ya tarehe 21 hadi 27 Machi 2016. Kwa wiki hii ya tarehe 28 Machi hadi 3 Aprili 2016 kulikuwa na jumla ya wagonjwa wapya 430 na vifo saba (7). Idadi ya vifo kwa wiki hii imeongezeka kutoka vifo vinne vilivyoripotiwa katika wiki iliyopita. Kwa wiki hii mikoa iliyopata wagonjwa wengi zaidi ni Kilimanjaro (128), Mara (102), Morogoro (67), Geita (46), Mwanza (40) na Dar es Salaam (31). Halmashauri kumi zilizoongoza kwa idadi ya wagonjwa wapya wiki hii ni Same (74), Tarime Vijijini (52), Moshi Vijijini (44), Mvomero (27), Rorya2

0 maoni:

Chapisha Maoni