Maeneo tulipo : Morogoro Road
Kimara Temboni Wilaya ya Kinondoni kabla ya Mbezi mwisho,
Saranga,hatua chache utaona kibao chetu barabara ni-Kushoto rangi ya
blue bahari.
6: Huduma zetu Kanisani:- Jumapili asubuhi saa 2:00 -4:30 watu wote kujifunza neno la Mungu ,Sunday School.
;saa 4:30-5:30 kusifu na kuabudu
na mambo mengine (ibada ya kawaida) 5:30-6:30 maombi ya udhihilisho wa
nguvu ya Mungu katikati ya kusanyiko (ibada) -kujazwa Roho Mtakatifu
(watu wote) -kunena kwa lugha mpya(watu wote) -kuponywa magonjwa
mbalimbali (watu wote) -kufunguliwa vifungo vya uovu vya asili,na
laana mbalimbali za watu (watu wote) 2: Jumatano: Hii ni siku ya
watumishi kuwepo Kanisani kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00
jioni kwaajili ya :- -Ushauri wa mtu mmojammoja (Canseling) -maombi
ya kufungua vifungo vya uovu kwa watu mbalimbali na laana
Mbalimbali -kuombea wagonjwa na kuponywa -kusikia shuhuda mbalimbali
kwa watu Mungu alivyo watendea. 3: Ijumaa siku hii ya ibada inaanza
saa 10:00- 12:00 jioni tunasifu na Kuabudu ,na kusikia neno la Mungu
,na Maombi.
Napenda kueleza kwa wale wenye
mapenzi mema kwa huduma yetu .Sisi tumepata bure Tunatoa bure watu hawa
tunao wahudumia ,au tulio wahudumia si matajiri ni watu wa kawaida kama
umeguswa na huduma yetu unaweza kuchangia huduma hii ili iwafikie watu
wengi zaidi.
Namba zetu za simu unaweza kutuma chochote,au kwa mazungumzo nasi Voda: 0767919056 – Tigo:0712964258 Airtel :0692567672.
Askofu E.A.Kalinga aliye simama
upande wa kulia katika picha, wakiwa katika picha ya pamoja na
Wachungaji. Baada ya kuwabariki katika Kanisa la Sinai Tanzania Mkoa
wa Rukwa, Sherehe hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa Serikali pia
,aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga mjini Meja Mstaafu Bahati Matala ambaye
wameshikana mikono kwa furaha pamoja na viongozi wa Kata ya Malangali
Wilaya ya Sumbawanga Mjini wakiwa pamojana baadhi ya niongozi wa
Kanisa.
Baadhi ya waumini ndani ya kanisa
wakijifunza neno la Mungu kipindi cha Sunday School ambacho kimekuwa
chenye baraka sana ya watu kulijua neno la Mungu kwa kina .
Askofu E.A Kalinga pamoja na mke
wake Mchungaji Christina Kalinga waliokaa viti vya mbele pamoja na
baadhi ya waumini wakiwa katika hafla ya pamoja wakisherehekea baada
ya ubatizo katika Kanisa hilo. Hili ni jambo linalo leta furaha katika
utumishi, baada ya kuwafundisha watu neno la Mungu na kuelewa na
kukubali kubatizwa.Math 28:19-20;Mark 16:15-16.
Waumini waliobatizwa wakiwa
katika picha ya pamoja na Askofu Kalinga na mke wake Mchungaji
Christina Kalinga , wakisherehekea baada ya ubatizo wao uliofanyika
kwa Mchungaji Sekela Mushi wa kanisa la Penuel lililoko Suka -Kimara
Dar es Salaam.
Askofu E.A Kalinga akimbatiza
Mmoja wa waumini waliokata shauri na kubatizwa na askofu huyo wa kanisa
la Sinai Dar es salaam kwa ubatizo wa maji mengi (kuzamisha).
Askofu .E.A.Kalinga kulia akiwa
katika picha ya pamoja na wanachuo wenzake wakati wa walipohitimu
shahada ya Diploma, katika chuo cha Bibilia cha The Oasis Healing
Bible College, kilichopo nyuma ya jengo la ubungo Plaza, karibu na
stendi ya mabasi yaendayo mikoani hapa Dar es Salaam.






0 maoni:
Chapisha Maoni