Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji
wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. Gabriel Nderumaki.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 14
Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi,
imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia tarehe 18
Machi, 2016.
Bi. Tuma Abdallah ni Mhariri Mtendaji Msaidizi wa Magazeti ya Serikali (TSN)
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
14 Aprili, 2016






0 maoni:
Chapisha Maoni