CHAMA
cha mpira wa miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) kimetauwa kamati ya
uchaguzi itakayohakikisha inasimamia chaguzi mbalimbali mkoani Iringa .
uchaguzi itakayohakikisha inasimamia chaguzi mbalimbali mkoani Iringa .
Uteuzi wa kamati hiyo unaelezwa kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa
kumaliza migogoro iliyoko ndani ya vilabu pindi wanachama wake
wanapotaka kuitisha uchaguzi lakini kunatokea migongano kati ya
wanachama na viongozi wao .
Akizungumza na mtandao huu wa kali ya Habari ofisini kwake Kaimu Katibu Mkuu wa
IRFA,Ramadhani Mahano alisema kuwa walifikia maamuzi hayo ya kuunda
kamati hiyo katika kikao cha wadau kilichoitishwa na mwenyekiti wake
Cypriyan Kuyava kilichofanyika juzi ili kumaliza migogangano ndani ya
vilabu .
Mahano alisema kamati hiyo itaongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni
GasterMdegela na makamu mwenyekiti akiwa ni Jakson Chaula .
Alisema kuwa kamati hiyo pia itakuwa na wajumbe sita ambao ni Lupyana
Masawa ,Willy Chikweo,Shemu Mhen pamoja na Happness Nduguru
Hata hivyo Mahano alibaimisha kuwa kamati hiyo pia itangozwa na
wanasheria wawili na wajumbe wake ni wanafamilia na wapenzi wa soka na
kamati hiyo itaanza kazi mara moja baada ya uteuzi wake .
Alisema licha ya kuunda kamati hiyo ya uchaguzi hapo awali chama
chake kililazimika kuunda kamati sita ikiwemo kamati ya Ligi na
Mashindano ambayo mwenyekiti wake atakuwa David Mwamalekela makamu
atakuwa Pascal Bella ambapo wajumbe watakuwa Carlo Mbinda, Gutram
Kawonga, Cletus Kifyoga, Nikolina Sanga, July Sawani na
Isiaka Majaliwa.
Mahano alisema kuwa Kamati ya Waamuzi itaongozwa na David Lugenge
akiawa na wajumbe Julias Mkomwa, Mwanaheri Kalolo, Abuu Yunus na
Atilio Mnyeke.
Alisema kwa upande wa Kamati ya Mipango na Uchumi mwenyekiti atakuwa
Stanford Mwakasala na wajumbe wa kamati hiyo watakuwa Abdallah
Kiyumbo, William Kessy, David Wapalila, Jonnie Nkoma, Daniel Kindole,
Rukia Muwango, Musa Kamtande na Victor Chakudika.
Alisema kuwa Kamati ya Maendeleo wanawake na Vijana, Mwenyekiti wake
ni Maulidy Toffy, huku wajumbe wakiwa ni Coster Magolosa, Tigana
Lukinja,Gift Mwachang’a,Edina Ndelwa,Thadeo Lukosina Haruna Mduda.
Mahano aliongeza kuwa kamati ya Nidhamu na Usuluhishi mwenyekiti
atakuwa ni Ignas Seboa Lutalemwa akifanya kazi na wajumbe Stanslaus
Matutu, Devotha Chaula na Fredrick Amando
0 maoni:
Chapisha Maoni