Marehemu
mwalimu aliyepigwa risasi akiwakinga wakristo wasiuawe na magaidi wa Al
Shabab ametuzwa medali ya juu zaidi na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais
Kenyatta alipokuwa akihutubia taifa alisema kuwa wale wakenya wachache
wanaoonesha ujasiri wa kukabiliana dhidi ya al shabab watatuzwa.
Na hivyo
akasema kuwa Mwalimu Farah ametuzwa heshima ya juu zaidi nchini Kenya
ya' Order Of The Grand Warrior', kwa ujasiri wake dhidi ya magaidi.
Marehemu
Salah Farah alikuwa katika basi lililokuwa likiwasafirisha abiria kutoka
mji mkuu wa Nairobi kuelekea Mandera walipotekwa na wapiganaji wa Al
shabab.
Punde wapiganaji hao wakaanza kuwagawanya waislamu na wale wasio waislamu.
Hapo
ndipo Mwalimu Farah na abiria wengine waislamu waliponga'amua nia ya
wapiganaji hao ilikuwa ni kuua wakristu , waliibua mbinu ya kuwakinga
abiria wakristo miongoni mwao ilikuokoa maisha yao.
Farah na wenzake wawili walijeruhiwa vibaya baada ya kukataa kugawanywa kwa makundi.
Kwa bahati mbata Mwalimu Farah alifariki mwezi Januari baada ya kuuguza majeraha ya risasi kwa takriban mwezi mmoja.
Tukio hilo la kijasiri lilichochea umoja miongoni mwa wakenya ambao wameshambuliwa mara kadhaa na magaidi wa Al Shabab.
Hiyo ilikuwa ni mara ya pili basi la kampuni hiyo ya Makkah kutekwa.
Mwezi Novemba mwaka uliopita wapiganaji wa Al Shabaab waliteka basi moja na kuwaua abiria 28 ambao hawakuwa waislamu.
Kundi
hilo liligonga vichwa vya habari mwezi Aprili mwaka uliopita lilipowaua
wanafunzi wakristo 148 katika chuo kikuu cha Garissa.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni