Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Iringa umewataka wazazi
na walezi kuwaingiza watoto wao katika mpango mpya wa huduma za
matibabu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18) unajulikana kwa jina
la “Toto Afya Kadi” kwa lengo la kuwawezesha watoto kuwa na uhakika wa
kupata matibabu wakati wote.
Kauli hiyo imetolewa na meneja wa bima ya afya mkoa wa Iringa dk
Mohamed Kilolile mapema leo hii wakati akizungumza na mtandao huu wa habari ofisini kwake ,alisema kuwa katika jitihada za kufikia lengo la afya
bora kwa watu wote ,Mfuko wa bima ya afya (NHIF)umetanua wigo wake na
sasa unasajili watoto katika huduma zake ili nao wapate huduma zao
pindi wanapokubwa na matatizo ya ugonjwa.
Alisema kuwa mara nyingi wazazi wamekuwa wakitumia garama kubwa katika
kuwahudumia watoto wao katika swala la afya na wakati mwingine kukosa
fedha kwa ajili ya kuwatibu watoto wao jambo linoloweza wakati
mwingine kusababisha kupoteza maisha lakini kwa kupitia huduma ya
toto afya kadi mtoto atatibiwa kwa mwaka mzima kwa shilingi 50,400/=
sehemu yoyote atakayopenda mwanachama .
Kiholile alisema kuwa hii ni fursaa nyingine ambayo imetolewa kwa
wazazi na walezi ambao ni wanachama wa mfuko lakini watoto wao
hawakusajiliwa kutokana na ufinyu wa nafasi za utegemezi kuwa ni
chache kwani mara nyingine mwanachama ana watoto sita lakini nafasi
zilizopo ni 4 hivyo wanapaswa kutumia fursa hiyo kusajili watoto wao
.
Alisema kuwa hii ni fursa ya kipekee pia kwa Watoto wanaoishi katika
mazingira magumu kupata Bima ya afya kupitia wafadhili na wahisani
mbalimbali ambao wangependa kuwasaidia ili pindi wanapopata matatizo
wawe na sehemu ya kupata Matibabu katika vituo Zaidi ya 600 nchi nzima
Kiholile alisema kuwa walengwa katika huduma hii ni watoto kuanzia
umri wa mika (18) kushuka chini kutoka katika makundi mbalimbali kama
watoto wote wa shule za awali, msingi na sekondari, Watoto wa kutoka
vituo vya kulea watoto yatima na wasiojiweza ,Watoto waishio na
wazazi/walezi bila kujali uhusiano walionao na kama wanasoma shule, au
hawasomi
Hata hivyo aliwataka wakazi wote wa mkoa wa Iringa kuchangamkia fursa
hiyo ya kipeke waliyokuwa wakiisubiri kwa muda mrefu kwa kuwandikisha
watoto wao ili wanufaike kwa pamoja na huduma hiyo .

0 maoni:
Chapisha Maoni