Hotuba ya taifa ya rais wa kenya Uhuru Kenyatta, imetatizwa kwa muda bungeni baada ya wabuge kadha wa upinzani kupuliza firimbi.
Wabunge hao walianza kupuliza firimbi na kuvuruga hotuba ya rais punde tu alipoanza kuitoa.
Ilimbidi spika wa bunge kuwasihi wabunge ambao walionekana kuendelea kupuliza firimbi.
Hata
hivyo utulivu ulirejea baada ya spika kuwatupa nje wabunge waliokua
wakizipuliza hizo firimbi, na rais akaendelea kutoa hotuba yake kwa
taifa.
0 maoni:
Chapisha Maoni