Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine
Mahiga (Mb.), akimpokea rasmi Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe.
Jean-Marc Ayrault (kushoto) alipotembelea Wizarani katika ziara yake ya
kikazi nchini. Mazungumzo kati yao yalijikita katika kuimarisha
ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa ili kuchangia maendeleo ya
nchi hizi mbili. Pia Waziri Mahiga alitumia fursa hiyo kumpa salamu za
pole kutokana na mashambulio ya kigaidi yaliyotokea nchini Ufaransa hivi
karibuni. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti,
2016.
|
Waziri Mahiga akizungumza huku Mhe. Waziri Ayrault akimsikiliza. |
|
Wajumbe
waliofuatana na Mhe. Waziri Aryault nao wakifuatilia mazungumzo. Kulia
ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Malika Berak. |
|
0 maoni:
Chapisha Maoni