Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Rahisi, (Easy
Banking), wa BancABC,Thompson Mwasikili, (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa
Kitengo cha Biashara cha benki hiyo, Joyce Malai, wakati akizindua huduma mpya ya “Mkoporahisi”, makao makuu ya benki hiyo
jijini Dar es Salaam, Agosti 2, 2016. BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara,
imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake ambapo mteja wa benki hiyo
ambaye ni mtumishi wa serikali anaweza kupatiwa mkopo ndani ya masaa 48
NA MWANDISHI WETU
BANCABC ambayo ni sehemu ya Atlas Mara
imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake kwani imeanza kutoa mikopo
ndani ya saa 48 kupitia huduma mpya ya ‘mkoporahisi’.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti
1, 2016, makao makuu ya benki hiyo, kwenye jingo la Uhuru Hights jijini Dares
Salaam, Mkuu wa kitengo cha Easy Banking wa BancABC, Thomson Mwasikili, (pichani juu), alisema
wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuwavutia wateja wengi zaidi kutoka sekta
mbalimbali ikiwemo serekalini ili kuhakikisha wanapata huduma hii kwa haraka.
“Kwa kupitia huduma hii ya mkoporahisi
tutahakikisha kuwa wateja wetu ambao ni waajiriwa wa Serikali, wanapata mikopo
yao ndani ya saa 48 kuanzia muda ambao maombi yaliwasilishwa..tutalisimamia
hili na kuhakikisha linatekelezeka,” alisema Mwasikili.
Bw. Mwasikili alisema benki yake inatoa
mikopo ya hadi Tsh milioni 40 kwa riba ya kiwango cha chini
hadi asilimia 1.6 kwa mwezi ambayo ni miongoni mwa riba za chini kabisa katika
soko la sasa.
“Waombaji wataweza kulipa mikopo yao kwa
muda mrefu wa hadi miaka 6 na hakuna pingamizi kuhusu lini unaweza kuongeza
mkopo wako,” alisema na kuongeza kuwa muombaji ana uhuru wa kupata mkopo wa
muda mfupi hata wa mwezi mmoja.
Kwa mujibu wa Mwasikili, tofauti na mikopo
mingine, waombaji wana uhuru wa kuchagua matumizi ya fedha kwa mfano kulipia
ada, kununua gari, kukarabati nyumba, kulipia kodi na kumaliza ujenzi na benki
haitamlazimisha mkopaji matumizi ya mkopo wake.
Waombaji pia watapata fursa ya kuchanganya
mikopo yao yote na kuwa na mkopo mmoja kwani BancABC inaweza kununua mikopo
yote hiyo na kumpunguzia mteja usumbufu.
“Endapo muombaji wa mkopo atafariki, mkopo
utafidiwa kupitia bima ya mikopo na fedha kiasi cha Tsh 500,000 taslimu
zitatolewa kugharamia mazishi,” alisema
“Tunatoa rai kwa wateja wetu wote na pia
wale ambao hawana akaunti na benki yetu kuchangamkia huduma hii ya mkoporahisi
kwani hii ndio benki pekee ambayo inakusogeza karibu na ndoto zako , pata
mikopo ndani ya saa 48,” alisema.
Atlas Mara iliorodheshwa katika soko la
hisa la London Disemba 2013. Atlas Mara ina lengo la kujitanua na kuwa kinara
katika masuala ya kifedha katika ukanda wa sub sahara kwa kutumia uzoefu wake
na uwezo wa kukuza mitaji. Malengo yake ni kuunganisha na kukuza uwezo wa
taasisi za kifedha na pia kuendeleza uchumi katika nchi ambazo inafanya
shughuli zake.
0 maoni:
Chapisha Maoni