Postedy by Esta Malibiche by on August 3, 2016 in BURUDANI with No comments
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey
and Clifford, Rashid Tenga alielezea machache mbele ya wageni na
waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo juu ya huduma mpya ya
matangazo katika bara la Afrika utakaowanufaisha watangazaji, wasanii na
watu maarufu uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu
wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole
Gabriel na Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Binary, Eni
Kihedu. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Katibu Mkuu wa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel
(katikati) akimsifia msanii Diamond Platinumz kwa jinsi ambavyo amekuwa
akiitanga Tanzania nje ya nchi kwa muziki wake.
Katibu Mkuu wa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole
Gabrielakimsifia Wema Sepetu jinsi ambavyo amekuwa akilitunza jina lake.
Msanii Diamond Platinuz akitoa shukrani zake za pekee kwa niaba ya wasanii walihudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey
and Clifford, Rashid Tenga (kushoto) akizunguza na Katibu Mkuu wa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole
Gabriel wakati wa uzinduzi wa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya
kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara
zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii iliyofanyika
jijini Dar es Salaam. Pembeni ni
Wageni waalikwa waliohudhuria shughuli hiyo.
Wasanii waliohudhuria shughuli hiyo.
Waandishi nao hawakuwa nyuma kufuatilia tukio.
Huduma ya matangazo kidigitali kwa kutumia wasanii na watu maarufu yaanzishwa nchini.
—
Kampuni inaoongozwa kwa kutoa
huduma ya matangazo ya biashara nchini ya Aggrey & Clifford
imezindua kitengo cha kutoa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya
kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara
zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii ambayo
itanufaisha pande zote zitazoshiriki kutumia huduma hii .
Huduma hii ya kisasa
inayoendana na wakati wa sasa wa kizazi kipya inawezesha matangazo
kuwafikia walengwa wengi na kwa haraka inasimamiwa na kampuni tanzu ya
masuala ya huduma za matangazo ya biashara kwa kutumia teknolojia ya
kidigitali ya Aggrey&Clifford inayojulikana kama Binary.
Uzinduzi wa kitengo hiki cha
matangazo kwa kutumia teknolojia ya kisasa itakayoleta mapinduzi katika
sekta ya matangazo ya biashara nchini umefanyika jana katika hoteli ya
Hyatt Regency ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel na
ilihudhuriwa na wataalamu wa masoko kutoka makampuni ya FMCG, huduma za
mawasiliano,mabenki na taasisi mbalimbali za biashara ikiwemo wasanii na
wanamichezo.
Kampuni ya Binary kwa kuanza
tayari inashirikiana na wasanii na watu maarufu Zaidi zaidi ya 40 ambao
miongoni mwao wapo wasanii wa filamu,wanamuziki,watangazaji maarufu wa
redio na luninga. Kutokana na ushirikiano huu Binary itawatumia katika
huduma za matangazo za wateja mbalimbali wanaotangaza huduma na bidhaa
zao kidigitali ili kuwafikia watumiaji wa huduma/bidhaa wengi na kwa
urahisi.
Huduma hii mpya ya matangazo
katika bara la Afrika unanufaisha watangazaji kwa huduma zao kuwafikia
wananchi ama wateja wengi kutumia umaarufu wa wasanii na watu maarufu
ambao pia wananufaika kwa kupata mapato ya uhakika kutokana na kutumiwa
kwao katika huduma ya matangazo na pia ina unafuu kulinganisha na njia
nyingine za matangazo.
Profesa Elisante Ole Gabriel
alisema kuwa serikali inao dhamira ya kuwasaidia wasanii wa tasnia
mbalimbali na wanamichezo na alipongeza kuanzishwa kwa huduma hii nchini
ambao itaongeza ajira na vipato vya wasanii wakati huohuo kunufaisha
makampuni kwa njia ya matangazo ya biashara zao.
Naye Mkurugenzi wa Ukuzaji
Biashara wa Binary, Eni Kihedu amesema “Huduma hii mpya ni jukwaa la
aina yake lya matangazo ya baiashara kwa kuwa inawezesha matangazo
kuwafikia walengwa kwa asilimia 100% kwa kulinganisha na kutangaza kwa
kutumia magazeti na ama majarida na inaleta unafuu kwa watangazaji ambao
kwa kutumia mtandao wasanii zaidi ya 40 ambao tunashirikiana nao
kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii matangazo yataweza kuwafikia
watumiaji wa bidhaa na huduma zaidi ya milioni 20 nchini na tunao uwezo
wa kufikia watu wengi zaidi”.
Kuhusiana na huduma hii mpya ya
matangazo itakavyonufaisha wasanii Kihedu alisema “Tunatumia fursa ya
kutumia teknolojia ya digitali katika biashara ambayo itaongeza vipato
vyao wakati huohuo vipaji vyao kuendelea kuonekana kwa watu wengi katika
jamii na kuwawezesha kuwekeza zaidi kwenye fani yao na tasnia yao”
Aliongeza kuwa ushirikiano wa
Binary na wasanii katika huduma za matangazo utafanyika kwa uwazi na
kunufaisha pande zote na kutafanyika makubaliano maalumu ya malipo
kutokana na viwango vinavyotozwa kwa kila tangazo litakalowekwa kwenye
akaunti za mitandao yao ya kijamii na kulingana na wafuasi wanaotembelea
akaunti zao.
“Viwango vya matangazo viko
wazi kwa watangazaji na wasanii hivyo tunaamini kila upande utanufaika
inavyostahili .Tunaamini njia hii ni jukwaa la aina yake kwa watangazaji
kufikisha matangazo yao kwa wateja wanaowalenga kwa kuwa njia
zilizokuwa zinatumika awali kutangaza hazina nafasi tena kutokana na
mabadiliko ya tekonolojia“.Alisema
0 maoni:
Chapisha Maoni