Postedy by Esta Malibiche on August 17.2016 inNews
Na: Lilian Lundo na Sheila Simba – MAELEZO
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ametoa siku saba kuanzia Agosti
17, 2016 kwa vyuo vikuu kurejesha fedha zilizopokea ambazo ni za
wanafunzi ambao hawapo chuoni.
Prof. Ndalichako ameyasema hayo
leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu
ya taarifa la zoezi la uhakiki wa wanafunzi wanufaika wa mikopo vyuo vya
Elimu juu.
Prof. Ndalichako amesema kuwa
uhakiki wa wanafunzi hao umefanyika katika vyuo 31 kati ya vyuo 81
vilivyopo nchini, Katika utafiti huo wanafunzi 2,192 wameshindwa
kuhakiki majina yao, hivyo kushindwa kuthibitisha uwepo na uhalali wa
wanafunzi hao.
“Mikopo ya Wanafunzi hao
imesitishwa na kwa wale ambao ni wanafunzi halali lakini walishindwa
kujihakiki itabidi waombe tena mkopo,” alifafanua Mhe. Ndalichako.
Ameendelea kwa kusema kuwa, kwa
mwaka wa fedha 2015/16 wanafunzi hao hewa wameigharimu Serikali kiasi
cha shilingi 3,857,754,460, kiasi ambacho kinatakiwa kurejeshwa na vyuo
ambavyo wanafunzi hao wamebainika.
Aidha, Prof. Ndalichako amesema
kuwa taarifa hiyo imekabidhiwa kwenye vyombo vya sheria ili kuwachukulia
hatua wale wote watakaobainika kufanya udanganyifu na kusababisha
Serikali hasara ya mabilioni ya fedha.
Vile vile Prof. Ndalichako
amewataka wakuu wa vyuo kuweka mfumo wa kuhakiki usahihi wa matokeo ya
wanafunzi yanayotumwa Bodi ya Mikopo kutokana na vyuo vingi kubainika
kuwepo kwa udanganyifu mkubwa kwenye matokeo ya wanafunzi ambao
hawakufanya mtihani au waliofeli na kuandikiwa wamefaulu ili waendelee
kupata mikopo.
0 maoni:
Chapisha Maoni