Postedy by Esta Malibiche on August 17.2016 in News with No comment
NA VICTOR MASANGU, RUFIJI
IMEELEWA kuwa nguvu kazi kubwa
ya taifa inapotea bure kutokana na baadhi ya vijana wengine nchini
Tanzania kuwa wavivu na kutojishughulisha na shughuli za kuleta
maendeleo na badala yake wanaamua kujiingiza katika makundi ya
uharifu,uvutaji wa madawa ya kulevya, pamoja na kupoteza muda mwingi
kushinda kutwa nzima wakiwa wamekaa vijiweni bila kazi yoyote.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa
wa Pwani Injinia Evarist Ndikiro wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa
programu ya kambi ya vijana ya kuwafundisha masuala ya kilimo na
maarifa ambayo ipo chini ya mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto
rufiji (RUBADA) iliyofanyika katika kijiji cha Mkongo.
Ndikilo amebainishwa kwamb
serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli
isingependa kuona vijana wa kitanzania hawataki kutumia fursa zilizopo
na kuamua kujiingiza katika vitendo ambavyo vipo kinyume kabisa na
taratibu na sheria zilizowekwa ambapo wakati mwingine zinaweza
kusababisha vurugu.
Naye mwakilishi wa shirika la
chakula duniani (FAO) nchini Tanzania Fred Kafeero amesema kwamba
kulingana na ripoti zinaonyesha asilimia 70 ya vijana katika africa
hawana ajira hivyo kunahitajika juhudi za makusudi za kuweza kuwasaidia
katika kilimo cha mboga mboga,huku Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Chwayo
akiwaomba vijana hao kutumia fursa ya kilimo kupitia mafunzo
watakayoyapata.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo
la Rufiji Mohamed Mchengerwa ameutaka uongozi wa RUDABA kuhakikisha
kwamba wanaepukana na malalamiko ambayo yalikuwa yanatolewa dhidi yao na
badala yake waweke mikakati endelevu ya kuwasaidia vijana kujiendeleza
zaidi pamoja na kuongeza juhudi za ujenzi wa viwanda kwa lengo la
kuweza kuongeza kasi ya maendeleo na kukuza uchumi.
Kwa upande wao baadhi ya vijana
ambao watanufaika na profamu hiyo akiwemo Saimoni Nyimmba pamoja na
Joseph Bada wamesema kwamba mafunzo hayo ya kilimo na maarifa pindi
watakapomaliza yataweza kuwasaidia kuwapatia kipato pamoja na kuachana
na suala la kuwa tegemezi sambamba na kuondokana na kile kilimo cha
kizamani.
MAFUNZO hayo ya kilimo na
maarifa yataweza kuwanufaisha vijana wapatao 200 kutoka mikoa mbali
mbali ya Tanzania ambapo kwa sasa yataanza kuwanufaisha vijana 62 kutoka
katika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo ujuzi watakaupata wataweza
kupata fursa ya kujiajiri wao wenyewe na kuleta mabadiliko chanya ya
kimaendeleo kupitia sekta ya kilimo.
0 maoni:
Chapisha Maoni