Postedy by Esta Malibiche on August 17.2016 in News
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akifungua mafunzo juu ya Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma, pembeni yake ni Kanimu Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bi. Lorah Madete.
Wakufunzi kutoka Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (wenye kompyuta mpakato), wa kwaza kutoka kushoto ni Dkt.
Kenneth Mdadila, Katikati ni Dkt. John Mduma, na kulia (mwenye tai) ni
Dkt. Jehovaness Aikaeli.
Kaimu Naibu katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bi. Lorah Madete Akionesha kitabu cha Mwongozo
wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya
Umma kwa wajumbe wa mafunzo (hawapo pichani), pembeni yake ni Kaimu
katibu Mtendani wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri.
Baadhi ya wajumbe Wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mafunzo.
………………………………………………………………
Na Adili Mhina
Tume ya Mipango imeanza zoezi la
kuwajengea uwezo wataalamu katika kuandaa na kutekeleza miradi ya
maendeleo inayotumia fedha za serikali au kwa kushirikiana na Sekta
binafsi kwa lengo la kuongeza nidhamu na weledi katika matumizi ya
rasilimali za Umma.
Mafunzo hayo yanayoendelea katika
moja ya kumbi za ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es salaam na kuendeshwa
na wataalamu elekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yanalenga
kuanda wataalamu ambao watakwenda kutoa mafunzo kwa maofisa wa Serikali
walio chini ya idara za Sera na Mipango na zile za uwekezaji katika
Wizara, Mikoa, Halmashauri, pamoja na mashirika na taasisi mbalimbali za
umma hapa nchini.
Akifungua mafunzo hayo mwanzoni
mwa Juma, Kaimu Katibu Mtendani kutoka Tume ya Mipango, Bibi Florence
Mwanri alieleza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuimarisha utendaji,
uwajibikaji na kuleta ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma
zinazoelekezwa katika miradi ya maendeleo.
“Shabaha kuu ya mafunzo haya ni
kutoa maelekezo ya mchakato na hatua zinazohitajika kufuatwa katika
kutayarisha na kutekeleza miradi yote inayotumia fedha za umma au kwa
kushirikiana na sekta binafsi,” Alisema Bibi Mwanri.
Kamu Katibu Mtendaji huyo alieleza
kuwa kutokana na kukithiri kwa kasoro katika miradi ya maendeleo
inayotumia fedha za umma, Serikali kupitia Tume ya Mipango ililazimika
kuandaa Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji
katika sekta ya Umma (Public Investment Management Operational Manual)
ambao utatumika katika kuandaa, kutekeleza na kusimamia miradi yote
inayotumia fedha za umma au kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Bibi Mwari alieleza kuwa katika
awamu hii ambayo Serikali imejikita katika kujenga uchumi wa viwanda
miradi mingi ya maendeleo inatarajiwa kuanzishwa. Hivyo, bila kuwa na
uelewa wa pamoja moingoni mwa wadau wanaohusika katika kuandaa,
kutekeleza na kusimamia miradi hiyo malengo ya Mpango wa Pili wa
Maendeleo hayatafikiwa kama inavyotarajiwa.
“Katika kipindi hiki ambapo bajeti
ya maendeleo imeongezeka na kufikia asilimia arobaini ni wazi kuwa
miradi mingi ya maendeleo inaanzishwa, hivyo ni lazima kila mtaalamu
aelewe kuwa tunawajibu wa kuandaa miradi bora, yenye tija kwa wananchi
na inayoendanda na thamani ya fedha zinazotumika,” Alisisitiza Bibi
Mwanri.
Bibi Mwanri aliwataka wajumbe wote kuhakikisha wanatumia mafunzo hayo vizuri ili kupata uelewa wa kutosha juu ya mwongozo huo.
Mafunzo hayo ya siku tano
yamehudhuriwa na wajumbe kutoka Wizara, Taasisi za Serikali, Wadau wa
Maendeleo, Asasi za Kiraia pamoja na Sekta binafsi na yanatarajiwa
kuandaa wataalamu bora watakaokwenda katika kanda mbalimbali nchini
kutoa mafunzo tarajiwa kwa walengwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni