Postedy by Esta Malibiche on Auugust 3.2016 in News
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akitoa maelekezo kwa
Meneja wa kiwanja cha ndege cha Rukwa Bw. Sandali Kaisi (kushoto) kuhusu uboreshwaji
wa kiwanja hicho wakati alipotembelea kiwanja hicho.
“Hakikisheni
baada ya wiki mbili vifaa vinakuwepo katika eneo la kazi na mnatekeleza wajibu
wenu kukamilisha barabara hii kwa wakati tuliokubaliana ili ianze kutumiwa na
wananchi”, amesema Prof. Mbarawa.
Waziri
Prof. Mbarawa ameongeza kuwa wananchi wanamatarajio makubwa na barabara hiyo
kwa muda mrefu hivyo Mkandarasi ahakikishe kazi ya ujenzi katika kipande
kilichobaki kwa kiwango cha lami inamalizika ifikapo mwezi Julai mwakani ili
kuharakisha shughuli za kimaendeleo mkoani hapo.
Aidha,
amemtaka mkandarasi huyo kukamilisha mzani wa kupima uzito wa magari katika kijiji
cha Kanondo KM 5 kutoka Sumbawanga mjini ifikapo mwezi Agosti mwaka huu kwa
lengo la kudhibiti uzito wa magari yanayofanya shughuli za kusafirisha mizigo
na abiria katika barabara hiyo.
|
|
Meneja wa kiwanja cha
ndege cha Rukwa Bw. Sandali Kaisi (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo ya hali ya
miundombinu kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
(kulia kwake) wakati Waziri alipokagua kiwanja hicho.
Kwa
upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Rukwa,
Eng. Masuka Mkina amemuhakikishia Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara zote
utazingatia viwango na utakamilika kwa wakati.
"Nikuhakikishie
kuwa tutasimamia na kuzingatia viwango vilivyowekwa katika mradi wa ujenzi huu ili
wananchi wanufaike na kuongeza uchumi wa mkoa ",amesema Eng. Mhina.
Ujenzi
wa barabara ya Sumbawanga-Namanyere-Mpanda kwa kiwango cha lami unagharamiwa na
Serikali ya Tanzania kwa jumla ya kiasi cha Shilingi bilioni 150.
|
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi
anayejenga barabara ya Sumbawanga Mjini-Chala- Kanazi yenye urefu wa KM 75 alipokagua
ujenzi wa barabara hiyo.
|
|
Mkandarasi anayejenga
barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni yenye urefu wa KM 76.6 akifafanua jambo kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati
alipokagua ujenzi huo. Katikati ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS)
Mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina.
|
|
Mbunge wa Jimbo la
Nkasi kaskazini Mhe. Ally Kessy akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea Jimboni kwake.
Mkandarasi
Jianx-Geo Engineering Group Corporation kutoka China anayejenga sehemu ya
barabara ya Sumbawanga Mjini-Chala-Kanazi kwa kiwango cha lami amepewa wiki
mbili kurejesha vifaa vya ujenzi katika eneo la kazi ili kuongeza kasi ya
ujenzi wa barabara hiyo ambao umeonekana kusuasua kutokana na ukosefu wa vifaa
vya kutosha.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa, wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa barabara ya
Sumbawanga-Namanyere-Mpanda Mkoani Rukwa.
Waziri
Prof. Mbarawa amesema barabara hiyo imegawanywa katika sehemu mbili ambazo ni
Sumbawanga Mjini-Chala-Kanazi KM 75 na Kanazi-Kizi-Kibaoni KM 76.6 ili
kuhakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati na viwango kulingana na
mkataba.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni