Mbunge
wa Jimbo la Kawe Mh. Halima James Mdee amesema asipotekeleza ahadi
alizoziadi katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana kwa
zaidi ya asilimia hamsini hatogombea katika uchaguzi wa 2020.
Mdee aliyasema hayo jana katika kipindi cha HotMix kinachorushwa na kituo cha EATV.
“Kama
sitatekeleza ahadi zangu kwa zaidi ya asilimia 50 sitagombea uchaguzi
kwa kuwa kama nitashindwa kuondoa kero za wapiga kura wangu sistahili
kuwa mwakilishi wao,” alisema.
Aliongeza
kuwa “Lazima nilipoishia katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
nipaendeleze ili hata nikisimama mbele ya wananchi wangu kuomba kura
watanipa kwa sababu sikuwaangusha.”
Alisema amefanikiwa kupunguza baadhi ya changamoto kwenye jimbo lake la Kawe ikiwemo migogoro ya ardhi, miundombinu na Maji.
“Kukijuwepo
na migogoro ya ardhi kwenye Maeneo ya Kunduchi, Mabwepande, na Bunju
lakini kwa sasa inapungua na wananchi wanapata hatimiliki ya ardhi,”
alisema.
“Kama mbunge siyo mfuatiliaji, haziwasilishi kero za wananchi wake Mahala husika, huyo hafai,” alisema.
Alisema mbunge lazima azifahamu siasa za ndani na nje ya nchi ili aweze kuisimamia serikali ipasavyo.
Ongeza: Mdee katika uchaguzi Mkuu wa 2015 aliogombea na Kipi Warioba ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi.
Na Regina Mkonde
0 maoni:
Chapisha Maoni