Kama
ukitaja habari ya michezo nchini ambayo inazungumzwa zaidi kwa sasa
huwezi kuacha kuitaja habari ya Yusuph Manji kujiuzulu nafasi yake ya
Uenyekiti wa klabu ya Yanga.
Maamuzi
hayo yanatajwa yalichukuliwa na Manji baada ya kuona kuwa anashutumiwa
vibaya na watu mbalimbali wakiwepo viongozi wa serikali na viongozi
wengine wa Yanga hivyo kukaa pembeni ili kulinda heshima yake.
Jambo
hilo lilionekana kupokelewa vibaya na mashabiki na wanachama wa Yanga
kwani Jumanne ya Agosti, 17 walikutana katika makao makuu ya klabu yao
na kukubaliana kumsimamisha uanachama Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa
Yanga, Ibrahim Akilimali ambaye alidaiwa ndiyo aliyechochea Manji
kuchukua uamuzi huo baada ya kuzungumza katika vyombo vya habari kuwa
Manji amekurupuka.
Baada
ya hayo yote, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa Yanga, Jerry Muro
ametoa taarifa kutoka kwa Manji ambayo amemwagiza aifikishe kwa
mashabiki wa klabu hiyo inayozungumzia hatma ya mahusiano yake na Yanga.
Kupitia
akaunti yake ya Instagram, Muro aliandika “Jerry waambie wana yanga
pamoja na vurugu zote hizi nitaendelea kuwa upande wao na kamwe
sitawaacha nguvu yangu iko kwa wanachama,wapenzi na mashabiki”- Bw Yusuf
Manji”
0 maoni:
Chapisha Maoni