Rais
wa Tanzania John Magufuli amependekeza daraja mpya la Kigamboni lipewe
jina la mwanzilishi wa taifa hilo Mwalimu Julius Nyerere.
Akiongea
muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi daraja linafaa kupewa jina la
Mwalimu Julius Nyerere kutokana na mchango wake kwa nchi hiyo.
Daraja
la Kigamboni lilianza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 kwa kuanza na
majaribio ambapo wananchai walianza kupita bure huku likiwa lina urefu
wa mita 680 na barabara unganishi upande wa Kurasini na Kigamboni zenye
urefu wa kilomita 2.5.
Ujenzi wake ulifanywa na kampuni ya China Railway 15 Group ikishirikiana na kampuni ya China Bridge Engineering Group.
Daraja
hilo ndilo la kwanza la kubeba uzito wa barabara kwa kutumia nyaya
Afrika Mashariki na la tatu Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara bila
kuhesabu Afrika Kusini.
Linamilikiwa
na serikali ya Tanzania na Hazina ya Malipo ya Uzeeni (NSSF) kwa 40% na
60% mtawalia na litachukua nafasi ya feri ya MV Magogoni.
0 maoni:
Chapisha Maoni