Hali
ya Usalama katika Kituo cha Afya cha Kata ya Buzuruga kilichopo
Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza imeimarika, baada ya Wakazi wa Kata
hiyo wanaounda Kikundi cha Kijamii cha “Ulipo Tupo” kufyeka vichaka
vilivyokuwa katika kituo hicho ambavyo vilikuwa vikitumiwa na wahalifu
kama maficho yao.
Baada ya kufyeka vichaka hivyo jumamosi iliyopita, Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Ndaisaba Aron
alisema kuwa vichaka hivyo vilikuwa hatarishi kwa wananchi, wagonjwa
pamoja na wahudumu wa Afya katika Kituo hicho, kutokana na kupata
malalamiko kwamba vibaka walikuwa wakikimbilia katika vichaka hivyo
baada ya kufanya uhalifu.
Hidaya
Bashiru ambae ni mwanachama wa kikundi hicho pamoja na Sixtus Ijugo
ambae ni Katibu, waliwasihi wananchi wengine kuwa na desturi ya
kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo katika maeneo mbalimbali
kama hospitali, shule na kwingineko kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe.
Diwani wa Kata ya Buzuruga, Richard Machemba, alijumuika na Kikundi hicho kwa ajili ya
kufanya
usafi katika Kituo hicho ambapo alipongeza juhudi mbalimbali
zinazofanywa na wakazi pamoja na vikundi mbalimbali vya maendeleo katika
Kata yake ambapo amewasihi wananchi kuendelea kujitoa kwa ajili ya
kushiriki shughuli za maendeleo.
0 maoni:
Chapisha Maoni