HALMASHAURI ya wilaya ya Kilolo imezinyoshea
kidole kaya zinazonuifaka na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ikiahidi kuziondoa
zile zinazotumia kwa ulevi na matumizi mengineyo yasiyokubalika, fedha
wanazopewa kwa ajili kugharamia
mahitaji ya msingi ikiwemo elimu, afya na maji.
Jumla ya kaya masikini 6,464 za halmashauri hiyo zinanufaika
na fedha za mpango huo zinazotolewa kila baada ya miezi miwili kupitia Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Mratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Kilolo, Venance
Mwaikambo alisema; “halmashauri yetu ilianza kunufaika na mpango huo toka Julai
mwaka jana na hadi mwezi Machi mwaka huu kaya hizo zilikuwa zimepata malipo ya
tano ya zaidi ya Sh Milioni 198 kwa ajili ya mwezi Machi na April.”
Wakati kaya hizo zikijipatia kati ya Sh 20,000 na Sh 70,000
kila baada ya miezi miwili, Mwaikambo alisema zipo taarifa zinazoendelea
kuchunguzwa zikihusisha baadhi yao kuzitumia fedha hizo kununua pombe na
matumizi ya starehe na michango isiyo ya lazima.
“Serikali haijaleta fedha hizi kama zawadi, inataka ziwatoe kutoka
hatua moja hadi nyingine,” alisema huku baadhi ya kaya zikikiri kuanzisha
miradi midogo midogo ya ufugaji na kilimo, kuwapeleka na kuwanunua watoto
mahitaji ya shule na kugharamia huduma za afya.
Mwaikambo alisema serikali haiwezi kukubali kuendelea kutoa
fedha kwa watu wanaozitumia kwa pombe na wamekwishapeleka maombi TASAF ya
kuwaondoa na kuziingiza kwenye mpango kaya nyingine mpya.
Afisa ushauri na ufuatiliaji wa mpango huo wa TASAF wilayani
Kilolo, Happy Mpuya alisema serikali kwa kupitia mpango huo inatoa ruzuku ya
msingi na ya masharti nafuu kwa kaya masikini ili kugharamia mahitaji ya msingi
ikiwemo elimu, afya na maji.
Mpuya alisema ruzuku ya msingi inatolewa kwa kila kaya iliyoandiskishwa kwenye mpango ili kugharamia mahitaji hayo ya msingi na ruzuku ya masharti nafuu inatolewa kwa kaya masikini zenye watoto wenye umri wa kwenda shule na kliniki.
Mpuya alisema ruzuku ya msingi inatolewa kwa kila kaya iliyoandiskishwa kwenye mpango ili kugharamia mahitaji hayo ya msingi na ruzuku ya masharti nafuu inatolewa kwa kaya masikini zenye watoto wenye umri wa kwenda shule na kliniki.
“Msije mkashangaa fedha mnazopata zinapungua kwasababu ya
mahudhurio hafifu ya watoto wenu shuleni na wale ambao wanatakiwa kupelekwa
kliniki hawapelekwi. Nataka mjue tuna utaratibu wa kufuatilia taarifa zenu za
jinsi fedha hizo zinavyowanufaisha,” alisema.
Alisema kaya zitakazobainika kuzitumia fedha hizo kinyume na malengo hayo zitaondolewa katika mpango kama masharti ya mpango yanavyotaka fedha hizo zisitumike kwa shughuli nyingine tofauti na za mpango.
Mmoja wa wanufaika wa mpango huo, Upendo Geufeni wa kijiji cha Itunda aliyepata jumla ya Sh 100,000 toka Julai mwaka jana alisema; “fedha hizo zinamsaidia kwa matibabu na akiba ndogo anayojiwekea imemuwezesha kufuga kuku.” alisema.
Dada huyo mlemavu aliiomba serikali kuboresha mpango huo kwa kutoa msaada utakaowawezesha kujenga nyumba bora.
0 maoni:
Chapisha Maoni