………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba hii leo amekutana na
kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Kamati ya Fedha ya Bunge la Finland.
Katika mazungumzo yao
yaliyofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Luthuli Dar es Salaam,
wabunge hao wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada inazofanya za
kulinda na kuhifadhi mazingira.
Awali, akiwakaribisha wabunge hao
Waziri Makamba amesema Tanzania inajivunia uhusiano mzuri uliopo baina
ya Tanzania na Finland na kuwashukuru wabunge hao kwa kufanya ziara
hiyo ya kikazi nchini Tanzania.
Waziri Makamba amesema Serikali ya
awamu ya Tano imejikita zaidi katika kuimarisha Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira ikiwa ni pamoja na kuandaa Mkakati Mkubwa wa Kitaifa wa
kupanda miti nchi nzima hususan maeneo kame ili kunusuru nchi na athari
za mabadiliko ya Tabianchi.
“Hivi sasa tuko katika hatua za
kuainisha maeneo yatakayopandwa miti hiyo kwa kuangalia aina za udongo
na miti itakayoweza kuhimili katika maeneo husika” Alisisitiza Makamba.
Waziri Makamba ameiomba Serikali
ya Finland kuendelea kushirikiana zaidi na Serikali ya Tanzania ili
kufikia malengo endelevu ya Uchumi na maendeleo ya Viwanda bila kuathiri
Mazingira.
Naye Balozi wa Finland Nchini
Tanzania Bw Mart Akhtsary aliyeambatana na ujumbe wa wabunge kutoka
Finland amemhakikishia Waziri Makamba kuendeleza na kudumisha
ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.






0 maoni:
Chapisha Maoni