Jumatano, 13 Aprili 2016

WATENDAJI WAONGOZA KWA KUOMBA RUSHWA PWANI


MLOW
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)mkoani Pwani imesema serikali ya mitaa katika mamlaka za watendaji wa vijiji ,mitaa na kata inaongoza katika vitendo vya rushwa huku wilaya ya Bagamoyo ikielezwa inaongoza kimkoa .
Aidha idara nyingine zinazoongoza katika vitendo hivyo ni sanjali na idara ya afya,polisi,mahakama,ardhi,sekta binafsi,elimu,tanesco,fedha,vipimo,uhamiaji na maji.
Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia jan hadi march mwaka huu,kwa waandishi wa habari jana,kamanda wa TAKUKURU mkoani hapo,Suzana Raymond ,alisema walipokea malalamiko 64 kwa kipindi hicho.
Alielezea kuwa kati ya malalamiko hayo malalamiko 49 yanahusiana na vitendo vya rushwa na uchunguzi wake unaendelea ambapo 15 kati ya yake hayahusiani na vitendo vya rushwa.
Kamanda Suzana alisema idara ya inayoongoza kwa malalamiko ya vitendo hivyo ni serikali ya mitaa ambayo ina malalamiko 18,ikifuatiwa na afya yenye malalamiko 8,polisi matano na Mahakama matatu.
Alitaja upande wa idara ya ardhi imelalamikiwa makosa matatu,sekta binafsi matatu,elimu mawili,tanesco mawili,fedha moja,vipimo moja,uhamiaji moja na maji moja.
“Watuhumiwa hao wengi wao wanalalamikiwa kwa kutumia vibaya mamlaka,kushiriki kuuza ardhi kinyume na taratibu,kutumia fedha za mapato ya kijiji ,mitaa na kata kiholel wakati ni matumizi mabaya ya fedha hizo”alielezea Suzana.
Alisema katika hicho jumla ya kesi mpya nne zilifunguliwa kwenye mahakama za wilaya na polisi huku kesi 22 zinaenelea kusikilizwa katika mahakama hizo.
Aidha kamanda Suzana alieleza kuwa katika kipindi cha july-sept mwaka 2015 kulikuwa na malalamiko ya vitendo vya rushwa 50 na octoba hadi desemba mwaka huo idadi ya vitendo vya aiina hiyo ilikuwa ni 45.
Hata hivyo taasisi hiyo mkoani Pwani katika kushughulikia kero za wananchi kwenye maeneo yanayoongoza kulalamikiwa ni kuendelea kufanya uchambuzi wa mifumo ili kubaini mianya ya rushwa na kutoa ushauri kwa idara husika na serikali kwa lengo la kuziba mianya iliyopo.
“Tunaendelea pia kutoa elimu kwa umma kwasasa tumekuwa na utaratibu wa kwenda vijijini kusikiliza kero na malalamiko”
“Kwa malalamiko ambayo hayahusiani na vitendo vya rushwa tunafikisha katika idara yenye dhamana pia idara itaendelea kufanya uchunguzi pale ushahidi utakapopatikana mtuhumiwa ama watuhumiwa watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake”alisema kamanda Suzana.
Akizungumzia suala la kutoa elimu katika jamii ,Suzana alisema ofisi yao ilielimisha jumla ya wananchi 4,443 kwa njia ya semina 47 na mikutano ya hadhara 11,kuimarisha klabu za wapinga rushwa 30 katika shule za sekondari na msingi mkoani humo.
Suzana alitoa wito kwa jamii kuwa kila mwananchi anapaswa kutambua anao wajibu wa kupambana na rushwa katika eneo lake kwa kukataa kutoa ama kupokea rushwa na kuwaomba watoe taarifa kwa taasisi mara wanapobaini kuna mtu anashiriki vitendo hivyo.

0 maoni:

Chapisha Maoni