Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), limewapongeza viongozi, mashabiki, wachezaji wa vilabu
na timu za Taifa kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ya
kimataifa iliyochezwa mpaka sasa.
Katika kipindi cha mwezi mmoja,
Tanzania imeshiriki katika michuano mbalimbali ya kirafiki, mashindano
ngazi za vilabu, timu za taifa ikiwemo ya Wanawake (Twiga Stars), Vijana
(Serengeti Boys) na Taifa Stars.
Katika michezo kumi iliyochezwa
mfululizo mpaka sasa, timu za Tanzania hazijapoteza mchezo hata mmoja
mpaka sasa, ikiwa ni kwa vilabu pamoja na timu za taifa za Wanawake,
Vijana na Taifa Stars.
Twiga Stars ilitoka sare ya bao
1- 1 dhidi ya Zimbabwe mchezo uliochezwa Harare, Yanga ikaifunga APR
mjini Kigali 2-1, kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 jijini Dar es salaa,
wakati Azam FC ilifunga Bidvest 3-0 Johanesburg na kuendeleza tena
ushindi wa 4-3 Azam Complex Chamazi.
Taifa Stars ikiwa mjini N’Djamena
ilibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chad katika mchezo wa kuwania
kufuzu AFCON 2017, Serenegti Boys ikiifunga The Pharaohs kutoka Misri
katika michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa (2-1), (3-1) michezo
iliyochezwa Uwanja wa Taifa na Azam Complex Chamazi.
Mchezo wa tisa wa kimataifa,
Yanga SC ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly katika mchezo wa Ligi
ya Mabingwa Afrika (CAF CL), huku Azam FC ikiibuk na ushindi wa mabao
2-1 dhidi ya Esperance ya Tunisia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho
barani Afrika (CAF CC).
TFF inawaomba wachezaji,
viongozi, wadau na Mashabiki kuendelea kupigana kusaka ushindi katika
michezo inayofuata na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ya
nchi.






0 maoni:
Chapisha Maoni