Na Lorietha Laurence-Maelezo
………………………….
Kampuni ya Kijapani inayofanya
shughuli zake nchini (Tricster) imeandaa shindano la wazo la biashara
litakalozishirikisha nchi tano za Afrika zikiwemo
Kenya,Rwanda,Zambia,Zimbabwe na Tanzania mwenyeji wa mashindano hayo
kwa mwaka 2016.
Akiongea na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam Meneja Mradi kutoka kampuni ya Afrika New
Business Development Department(DMM) Bw.Alex Kapungu ambao ndio
wadhamini wa shindano hilo ameeleza kuwa lengo la shindano hilo ni
kusaidia kuboresha ujasiriamali katika bara la Afrika.
“Shindano hili linafanyika kwa
mara ya kwanza na hivyo ni fursa nzuri kwa wajasiriamali na wale
wanaotaka kuwa wajasiriamali kushiriki na baadaye kufanikisha wazo hilo
kiutendaji kwa kuwa biashara halisi”alisema Bw.Alex.
Aidha ameongeza kuwa vigezo vya
kushiriki shindano hilo ni mshiriki awe amefikisha miaka 18 na
kuendelea, awe anajua kuongea na kuandika lugha ya kiingereza na kuwa na
hati ya kusafiria.
Naye Mkurugenzi wa Trickster
Bw.Sonobe Atsushi amesema washindi watakaoingia nusu fainali watapata
fursa ya kutembelea nchi ya japani ambapo mshindi wa kwanza atapata
fedha taslimu Dola elfu tano za kimarekani.
Pia ametoa wito kwa watanzania
kujitokeza na kushiriki kwa wingi ili wapate fursa ya kuanzisha biashara
kupitia mawazo watakayoyatoa na hivyo kupanua wigo wa biashara.






0 maoni:
Chapisha Maoni