Jumatano, 13 Aprili 2016

Dkt.Kigwangalla akagua Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong’oto iliyopo Mkoani Kilimanjaro





DSC_0572
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitia saini kitabu cha wageni katika Hospitali ya  Taifa ya Kifua Kikuu Kibong’oto ilipo Mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake   10 Aprili 2016. Anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga.
DSC_0607
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo ya kitaalam kutoka kwa msimamizi wa Maabara ya Hospitali hiyo ya Kibong’oto
DSC_0608
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipatiwa maelezo ya kina namna ya vifaa hivyo vinavyofanya kazi katika upimaji wa kifua kikuu kutoka kwa  Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga
DSC_0612
Eneo la Utafiti wa magonjwa ya kuambukiza katika Hospitali hiyo ya KIbong’oto.
DSC_0611
….Wakitoka katika jengo la Utafiti
DSC_0599
Msafara ukielekea upande wa wadi za wagonjwa wa TB sugu..
DSC_0575
Moja ya alama zinazoelekeza maeneo ya Hospitali hiyo
DSC_0577
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Kibong’oto, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga akimuongoza Naibu Waziri wa Afya na watendaji mbalimbali kuelekea katika eneo wanalohudumia wagonjwa wenye Kifua kikuu (TB) sugu.
DSC_0581
Wafanyakazi wa Hospitali hiyo ya Kibong’oto na wageni wengine wakielekea katika eneo la TB sugu wakati wa ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Afya.
DSC_0579
Mkuu wa wilaya ya Siha,Dkt Charles Mlingwa (katikati) wakielekea katika eneo hilo la TB sugu wakati wa ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Afya.
DSC_0582
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipatiwa maelezo ya kina juu ya wagonjwa wa TB sugu waliopo ndani ya wodi (hawapo pichani) kutoka kwa  Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga.
DSC_0586 DSC_0584
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga akionyeshaa  namna wodi hizo zinavyofanya kazi na jinsi wanavyotoa huduma.
DSC_0595 DSC_0597
Msafara huo ukirejea katika maeneo mengine wakati wa ukaguzi  na Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla. Pichani wote waliovaa ‘mask’ maalum  ni kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya vijidudu vya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) hasa kwa upande huo wa wagonjwa maalum wa TB sugu.ambao wapo upande maalum. Hivyo kuvaa kifaa hicho kinasaidia kupunguza hali ya maambukizo wakati wa kufika eneo hilo kama sheria na taratibu zilizowekwa kitaalam na uongozi wa Hospitali hiyo.
DSC_0616
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo mafupi kutoka kwa wataalam wa Hospitali hiyo.
DSC_0620
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo mafupi kutoka kwa wataalam wa Hospitali hiyo.
DSC_0631
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa maagizo kwa uongozi wa Hospitali hiyo.
DSC_0637
Mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza, wa Hospitali ya Kibong’oto ,Dkt. Stella Mpagama  akimkabidhi  kitabu chake Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla.  (Picha zote na Andrew Chale,]



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla, ametembelea Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong’oto  eneo la Sanya Juu  Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro.
Dkt. Kigwangalla katika Hospitali hiyo, alipata kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu (TB)  ya kawaida na ile kali ambapo pia aliweza kutembelea  eneo la kituo cha utafiti cha magonjwa hayo pamoja na maabara.
Kihistoria Hospitali hiyo ya Kibong’oto ilifunguliwa rasmi 29 Oktoba mwaka 1952 na Lady Twining, baada ya miaka saba ya vita ya pili ya dunia chini ya utawala wa Muingereza na imekuwa ikitoa huduma hiyo ya magonjwa ya kuambukiza hususani Kifua Kikuu.
 Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga  amemwelezea Naibu Waziri changamoto mbalimbali ikiwemo suala la nyumba za watumishi na mambo mengine ikiwemo suala la bajeti ya vifaa tiba.

0 maoni:

Chapisha Maoni