Mchezo kati ya timu hizo za vijana
utachezwa kesho Jumanne saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki
na Kati, katika uwanja wa Azam Complex uliopo eneo la Chamazi jijini
Dar es salaam.
Katika mchezo wa kirafiki wa awali
uliochezwa Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
Serengeti Boys waliibuka na ushindi wa mabao 2 – 1 dhidi ya The Pharaos,
mabao ya Serengeti yakifungwa na kiungo Cyprian Bennedictor na Ally
Hussein.
Kikosi cha Serengeti Boys
kinachonolewa na makocha Bakari Shime na Sebastian Mkomwa wakishauriwa
na Kim Paulsen, baada ya mchezo wa awali kimeendelea na mazoezi katika
uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo huo wa kesho.
Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu
ya maaandalizi kwa timu zote Tanzania (U17) na Misri (U17) zinazojiandaa
na michezo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana
mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Madagascar.
Serengeti Boys itaanza kutupa
karata yake dhidi ya Shelisheli Juni 25, 2016 katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam na marudiano kuchezwa baada ya wiki moja nchini
Shelisheli.






0 maoni:
Chapisha Maoni