………………………………………………….
KAMPUNI ya kutengeneza chuma ya
Kamal Steel Ltd, imetoa msaada wa viungo bandia, kwa watu wenye ulemavu
16, vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 80.
Akifunga kambi ya kutoa viungo
bandia hivyo, jana jijini Dar es Salaam sambamba na kukabidhi vifaa
hivyo, Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema,
serikali itaendelea kuwawezesha watu wenye ulemavu nchini ili waweze
kukabiliana na changamoto zinazowazungika ikiwa ni pamoja na kuwapatia
vifaa bandia.
Alisema, suala la ulemevu linagusa maisha ya kila mwanadamu na kwamba mtu yoyote anaweza kufikwa na tatizo hilo.
Alibainisha, viungo bandia
vinauzwa kwa ghala makubwa ambayo watu wengi wenye ulemavu hawawezi
kumudu kununua hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau wake
itaendelea kutoa msaada wa vifaa hivyo.
“Jamii iamini kuwa wote ni
walemavu watarajiwa. Kupoteza kiungo kimoja cha mwili ni changamoto
kubwa. Tunaishukuru kampuni ya Kamal Steel kwa kutoa misaada hii
muhimu ambayo tunaamini kuwa inasaidia kupunguza madhira ya
ulemavu,”alisema Dk. Mwakyembe ambaye kupitia msaada huo ameweza
kuwasaidia watu wenye ulemavu wanne kutoka jimbo lake la Kyela mkoani
Mbeya.
Mwenyekiti wa makampuni ya Kama
Group , Gagan Gupta, alisema,kampuni yake haijatoa viungo bandia hivyo
kama msaada, bali kama wajibu wake kwajamii.
“Tunaamini kwamba, viungo hivi
bandia vitawawezesha kumudu kutembea, kufanya kazi mbalimbali zitakazo
waletea kipato,”alisema Gupta.
Katika hatua nyingine, Gupta
aliahidi kumuajiri mmoja wawatu hao wenye ulemavu mwenye taaluma ya
ufundi mitambo, Siaga Raphael ambapo alisema ajira yake itaanza leo.
“Huyu atafundishwa ufundi wa
kutengeneza vifaa mbalimbali hasa vya watu wenye ulemavu hapa, ili aweze
kusaidia kuwafundisha watu wenye ulemavu wengine.Mradi anataaluma hiyo
ataanza kazi kesho asubuhi (leo asubuhi),”alisema Gupta.
Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel,
Sameer Gupta, alisema, kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika
kusaidia viungo hivyo bandia kwa watu wenye ulemavu ambapo mpaka sasa
imesaidia watu 200.
“Tutaendelea kuwasaidia kila
mara ili tuweze kuisaidiana na serikali yetu kuwaondolea changamoto
wenzetu hawa. Tunaamini wakipewa viungo hivi bandia wanaweza kushiriki
shughuli mbalimbali muhimu zitakazowaingizia kipato,”alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake
walio pokea msaada huo, Siaga Raphael, aliipongeza kampuni hiyo kwa
masaada wa vifaa hivyo na kuitaka serikali kuwa kumbuka watu wenye
ulemavu kwa kuwasaidia pia kuwapa taaluma ya ufundi itakazowawezesha
kujimudu kimaisha.
0 maoni:
Chapisha Maoni