Posted by Esta Malibiche on Nov 4,2016 in NEWS
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akimpa maelekezo Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Bw Clemence Mkusa juu ya ujenzi wa zahanati ya kata ya Chang’ombe wakati alipotembelea eneo ambalo zahanati itajengwa wakati wa ziara yake aliyoifanya katika kata ya Chang’ombe iliyofanyika terehe 03 Novemba, 2016.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo
akimpa maelekezo Diwani wa kata ya Chang’ombe Bw. Bakari Fundikira juu
ya ujenzi wa soko jipya la Chang;ombe wakati alipofanya ziara ya kukagua
shughuli mbalimbali zinazotekelezwa katika kata hiyo iliyofanyika
tarehe 03 Novemba, 2016.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo
akipokea taarifa za maendeleo ya ujenzi wa soko la Chang’ombe B kutoka
kwa Mtendaji wa kata ya Chang’ombe Bi. Asha Juma wakati alipofanya ziara
ya kukagua ujenzi wa soko jipya la Chang’ombe B unaofanywa katika kata
ya Chang’ombe mjini Dodoma aliyoifanya leo tarehe 03 Novemba, 2016.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo
akiwapa mikono wanafunzi wa shule ya msingi Chang’ombe baada ya kuwapa
taarifa juu ya ujenzi wa madarasa na ukarabati wa majengo ya shule yao
wakati wa ziara aliyoifanya katika shule hiyo leo tarehe 03 Novemba,
2016.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani
Jafo akikagua jengo la ofisi ya Mtendaji wa kata ya Chang’ombe
linaloendelea kujengwa wakati wa ziara aliyoifanya katika kata ya
Chang’ombe kukagua shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazofanywa
katika kata hiyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani
Jafo akiwasalimu wanafunzi wa shule ya msingi Chang’ombe B iliyopo mjini
Dodoma wakati alipofanya ziara ya kukagua shughuli mbalimbali za
kimaendeleo zinazofanywa katika ziara hiyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo
akipokea taarifa za maendeleo ya ujenzi wa shule ya Msingi Chang’ombe B,
iliyopo katika halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kutoka kwa Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo Bi.Nelly Kinyaga alipotembelea shuleni hapo wakati
alipofanya ziara ya kukagua shughuli mbalimbali za kimaendeleo
zinazofanywa katika kata hiyo.
Na. Nasra Mwangamilo, Silvia Hyela
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameuagiza Uongozi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Dodoma kuhakikisha inakamilisha ujenzi na ukarabati wa
vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Chang’ombe, ifikapo tarehe 10
Januari, 2017 kabla ya msimu wa masomo kuanza.
Mhe. Jafo alisema serikali kupitia
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) imetoa
jumla ya shilingi Milioni 192 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 8 vya
madarasa na ukarabati wa majengo machakavu katika shule ya msingi
Chang’ombe na kuwataka watendaji hao kutumia vizuri fedha hizo
zilizotolewa na serikali.
Mhe. Jafo alitoa agizo hilo leo
tarehe 03 Novemba, 2016 wakati alipofanya ziara ndogo ya kutembelea Kata
ya Chang’ombe ambapo katika ziara hiyo alibaini changamoto mbalimbali
zinazoikabili shule hiyo zikiwemo upungufu wa madarasa na matundu ya
vyoo.
“Natoa agizo kwa Afisa Mipango na
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa, ifikapo tarehe 10 Januari, 2017, ujenzi wa
majengo haya uwe umeshakamilika na muhakikishe shule yote inakuwa mpya.
” Alisisitiza Mhe. Jafo.na kuongeza kuwa angependa kazi hiyo ifanyike
ndani ya muda na kutojengwa chini ya kiwango cha ubora.
Aidha, Naibu Waziri Jafo
alionyesha kutoridhishwa na taarifa za ujenzi wa zahanati ya kata ya
Chang’ombe ambayo taarifa zilizotolewa zilionyesha kuwa hazikuwa sahihi
ukilinganisha na idadi ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa
zahanati hiyo.
“Sijaridhishwa kabisa na ujenzi
unaoendelea katika zahanati hii na siamini kama kulikua na usimamizi
mzuri, nataka niletewe taarifa inayoambatana na taarifa ya mkandarasi
aliyehusika na ujenzi pamoja na mchakato wa manunuzi ya vifaa na
maendeleo ya ujenzi ili nijiridhishe na suala hili ”aliagiza Naibu
Waziri Jafo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Jafo
alipata nafasi ya kuzungumza na watumishi wa Manispaa ya Dodoma na
kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia umuhimu wa mahitaji ya wananchi na
kuyawekea kipaumbele mambo ya msingi ikiwamo huduma za afya na elimu
lengo likiwa ni kuhakikisha watumishi wa Serikali za Mitaa wanakua
watumishi wa mfano kwa utendaji mzuri.
0 maoni:
Chapisha Maoni