Jumatano, 16 Novemba 2016

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) LANG’ARA MAOYESHO YA WADAU WA BIMA DAR


 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga  (kushoto) akisisitiza  jambo  wakati wa maonyesho ya wadau wa bima  yaliyoandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) yanayofanyika  kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam,   wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bima ya Mgen  Charles Sumbwe , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya G A  Tanzania, Amit Srivastavr na Mkurugenzi Mtendaji wa kamapuni ya Bima ya Maxinsure, Bhaskar Nair.
Mmojawa wananchi aliyefika kwenye manesho ya wadau wa bima   Gudumo Gaironga(kushoto) akimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga  (kulia)  alipokuwa akimfafanulia jambo  wakati wa maonyesho ya wadau wa bima  yaliyoandaliwa na Taasisi ya Bima
Tanzania (IIT) yanayofanyika  kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Kamishina wa  wa Bima Tanzania  Ezraell Kamuzora (kulia) akiwapongeza wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)    pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wao Sam Kamanga  (kushoto)   wakati alipotembelea banda lao lililopo kwenye maonyesho ya wadau wa bima  yaliyoandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) yanayofanyika  kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam


 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga  akimpongeza mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) anayesoma kozi ya maswala ya bima Baraka Dinis  kwa kujitolea kutoa damu kwa ajili ya kuchangaia  Mpango wa Taifa wa Damu salama kwenye maonyesho ya wadau wa bima  yaliyoandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) yanayofanyika  kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Elisante Maleko.

0 maoni:

Chapisha Maoni