Nchi
inakwenda katika uchumi wa viwanda ambavyo vinahitaji wataalam
mbalimbali katika kuweza kufikia uchumi huo kwa kuhitaji wataalam
wanaozalishwa nchini wakiwemo wahitimu wa mafunzo stadi yanayotolewa na
vyuo vya VETA.
Hayo
ameyasema leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi
Stadi (VETA), Geoffrey Sabuni wakati wa mahafali ya 46 katika Chuo cha
VETA, Changombe Dar es Salaam, amesema VETA inazalisha wataalam ambao
wamebobea kwa ujuzi.
Amesema
wahitimu wa VETA hawatafuti ajira kutokana na kuwa ujuzi wanaoupata
unawawezesha kujiajiri au kuajiriwa kwa kutafutwa na wamekuwa wakifanya
vizuri katika maeneo walioajiriwa na kujiajiri.
Mkuu wa Chuo cha VETA, Chang’ombe, Douglas Kipokola akitoa maelezo katika mahafali ya 46 ya chuo hicho jijni Dar es Salaam.
Sabuni
amesema wanaosoma VETA wapo waliohitimu kidato nne hadi waliopata
shahada ya kwanza hivyo jamii iondoe dhana ya kwamba wanaosoma VETA ni
wale walioshindwa kufanya vizuri katika shule za sekondari na msingi.
Aidha
amewataka wahitimu wanaozalishwa na vyuo hivyo kuwa na weledi katika
kufanya kazi na kuondokana kuwaibia waajiri hali ambayo itafanya baadhi
yao kupoteza sifa ya kujiajiri au kuajiliwa.
Nae
Mkuu wa Chuo cha VETA Changombe, Douglas Kipokola amesema kuwa
wahitimu mwaka huu wako 423 katika fani mbalimbali na kwamba wapo
tayari katika soko la ajira kutokana na mafunzo walioyapata.
Amesema
kuna changamoto za walimu ambapo wameshaanza kulifanyia kazi kutokana
na mitaala inahitaji mafunzo yenye tija kwa uwiano wa mwalimu mmoja
kwa wanafunzi wasiozidi 20.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA , Geoffrey Sabuni akizungumza katika mahafali ya 46 katika Chuo cha VETA, Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu VETA , Geoffrey Sabuni akitoa cheti kwa mmoja wa
wahitimu katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe jana jijini
Dar es Salaam.
Wahitimu
wakiimba shairi kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) katika Mahafali ya 46
ya Chuo cha VETA, Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahitimu wakati wa Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wazazi katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni