Wajumbe
wa Kamati ya Urasimishaji kuhusu sekta ya Ubunifu wakiimba wimbo wa kuhamasisha
ushirikiano katika warsha iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania ambapo mada
mbalimbali ziliwasilishwa na wawezeshaji leo Jijini Dar es Salaam.
Picha/Habari Na
Lorietha Laurence
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura
ameitaka kamati ya urasimishaji sekta za ubunifu kuweka mfumo rasmi wa
kuwatambua wadau wa sekta hizo ili waweze kuwasimamia.
Mhe.
Anastazia ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua warsha
iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania ambapo alieleza kuwa kwa kuwepo kwa
mfumo rasmi wa kutambaua sekta hizo
kutarahisisha kuwatambua wasanii katika makundi mbalimbali.
“Sekta
ya ubunifu ni pana na muhimu katika kukuza pato la mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla
hivyo ni muhimu kurasimisha kwa kuwepo mfumo rasmi wa kuitambua” amesema Mhe.
Anastazia.
Anaongeza
kuwa kwa kutambua umuhimu wa sekta ya ubunifu Rais wa awamu ya tano Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli aliamua kufuata ilani ya chama cha Mapinduzi katika kuunda
Wizara ambayo inajihusisha na mambo ya sanaa.
Naye
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru
Millao amesema kufuatia warsha hiyo anaamini itasaidia kamati ya urasimishaji
kujipanga katika kusimamia kazi za filamu na muziki ili kuwa ajira rasmi yenye
kuingizia watu kipato.
“Mbali
ya sekta hii ya ubunifu kuwa rasmi pia
itasaidia katika kusambaza elimu kwa umma kuhusu mchango unaofanywa na sekta hiyo
katika kukuza uchumi na kuongeza ajira nchini” alisema Bibi. Nuru.
Aidha
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo ameeleza kuwa
warsha hiyo ipo katika kuwajengea uwezo wanakamati katika kuimarisha uelewa na
kuifanya sekta ya ubunifu kuwa rasmi.
Kwa
upande wake Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Mona Mwakalinga
amefurahishwa kuona Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inathamini
mchango wa kazi zote za ubunifu kwa kutaka kuzirasimisha kwani kwa kufanya hivyo
itasaidia kuinua kazi za ubunifu na kuzifanya kutumika zaidi nje ya nchi.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni