Posted by Esta Malibiche on Nov 17,2016 in NEWS
Mkuu wa Wilaya ya Arusha ametoa
angalizo kwa wananchi wote kuhusu tahadhari ya mlipuko wa ugonjwa wa
kipindupindu ambao umeripotiwa kuwepo katika Mikoa mbalimbali na maeneo
ya jirani na Wilaya hii.
Akizungumza kwenye kikao maalumu
na watendaji wa Kata, Maafisa Afya pamoja na wadau wa Afya Kaimu Mkuu wa
Wilaya ya Arusha Mhe. Alexander Mnyeti ameelezea hatua ambazo Serikali
ya Wilaya imechukua hadi hivi sasa kudhibiti mlipuko wa ugonjwa kuwa ni:
- Kuandaa kambi maalumu kwa ajili ya wagonjwa watakaojitokeza –ipo katika Kituo cha Afya Levolosi
- Kuagiza dawa na vifaa tiba kwa ajili ya tahadhari ya ugonjwa
- Kusambaza mabango, vipeperushi na miongozo katika vituo vua kutolea huduma za afya, Ofisi za Kata na mitaa pamoja na maeneo ya mikusanyiko
- Kufanya kikao na wadau wote na kuunda timu ya usimamizi wa mlipuko wa kipindupindu.
Kupitia kikao hiki kwa kauli moja wajumbe walikubaliana hatua za kuchukua ili kupambana na mlipuko:
- Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi kwenye maeneo yote yenye uhaba wa maji
- Kuchukua Sampuli za maji katika Kata za pembezoni
- Kupiga marufuku uuzaji wa matunda yaliyomenywa,vyakula barabarani na pombe za kienyeji
- Kutembelea kaya na kukagua uwepo wa vyoo na matumizi yake
- Kugawa vidonge vya Kutibu maji kwenye kila Kaya
- Kuwachukulia hatua wote watakaokiuka wa kanuni za Afya
Pia wananchi walishauriwa kujikinga na ugonjwa huu kwa njia zifuatazo;
- Kunywa maji yaliyochemchwa au yaliyowekewa dawa ya kuua vimelea
- Kula chakula cha moto kilichotayarishwa katika hali ya Usafi.
- Kunawa mikono kwa sabuni na maji ya kutitirika (usinawe ndani ya chombo).
- Kuhakikisha matumizi bora ya choo na kinyesi cha watoto wadogo kitupwe chooni
- Kuepuka kula matunda bila kuyaosha na kunywa juisi na vyakula vinavyouzwa kiholela.
IMETOLEWA NA
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha.
17 Novemba ,2016
0 maoni:
Chapisha Maoni