Jumamosi, 26 Novemba 2016

MKUU WA MKOA AKERWA NA NAMNA JIJI LA MBEYA LINAVYOSHUGHULIKIA KERO ZA ARDHI

Posted by Esta Malibiche on Nov 26,2016 in NEWS

MKUU wa Mkoa wa Mbeya amemwagiza mkurugenzi wa jiji la Mbeya kuandaa mpango kazi wa kumaliza tatizo katika idara ya ardhi ikiwemo ucheleweshaji wa ulipaji fidia na kuwapatia viwanja wananchi wote waliowapa hati na sasa wanazungushwa bila kupatiwa viwanja.

Hayo ameyasema Leo katika utaratibu wake aliouweka tangu ateuliwe wa kusikiliza Kero za wananchi kila siku ya alhamisi YA mwanzo wa mwezi na Alhamisi ya wiki ya  mwisho wa mwezi ambapo asilimia 90 YA malalamiko yanahusu Ardhi.


Aliwataka watendaji wa Ardhi kubadilika na kuwa Karibu na wananchi na kushughulikia kero zao kwa haraka. 


Makalla mehaidi kufuatilia kwa Karibu utendaji kazi wa idara ya Ardhi ili itatue kero za wananchi.Pia
amemwagiza mkurugenzi wa jiji kuwasilisha mpango kazi wa kumaliza tatizo la Ardhi


  Mamia YA wananchi waliojitokeza siku ya kusikiliza  kero wadai wanazungushwa kuonyeshwa viwanja wakati wamepewa hati










0 maoni:

Chapisha Maoni