Jumamosi, 26 Novemba 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA ATEMBELEA KIWANDA CHA A TO Z MKOANI ARUSHA

Posted by Esta Malibiche on Teknolojia

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia nguo zinazotengenezwa na Kiwanda cha A to Z,kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw.Kalpesh Shah. Makamu wa Rais amefanya ziara kwenye kiwanda hicho ikiwa sehemu yakutambua mchango wa wawekezaji wa ndani na changamoto wanazokutana nazo ili kupata majibu ya kurahisisha kufanikisha Tanzania mpya ya Viwanda.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia namna  nguo zinazotengenezwa na Kiwanda cha A to Z kilichopo Kisongo mkoani Arusha,kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw.Kalpesh Shah.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna kiwanda cha A to Z kinavyofanya utafiti wa kupambana na wadudu wanaoharibu Mahindi kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha utafiti cha Africa Technical Research Centre Dkt.Johson Ouma Odera.
                                 …………………………………………………………………………… 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuviimarisha vyuo vya ufundi stadi nchini –VETA- ili viweze kutoa wahitimu bora ambao watakidhi katika soko la ajira hasa kwenye viwanda vilivyopo na vitajengwa nchini.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo wakati anazungumza na uongozi wa kiwanda cha A to Z kilichopo
mkoani Arusha katika ziara yake ambayo imeingia siku ya Pili ya kutembelea viwanda mbalimbali mkoani humo ili kujua changamoto zinazokabili viwanda hivyo na serikali kuzitafutia ufumbuzi.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali imetenga fedha za kutosha zitakazotumika kuviimarisha vyuo vya Veta
ili viweze kutoa mafunzo bora yatakayosidia vijana kufanya kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu pindi watakapoajiriwa au kujiajiri wenyewe.

Kuhusu maslahi kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha A to Z,Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kulinda na kutetea haki za wafanyakazi kwa kutoa maslahi mazuri ambayo yatawezesha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii.
Makamu wa Rais pia amesisitiza usawa katika ulipaji wa mishahara kwa wafanyakazi wa ndani na wa nje ya nchi walioajiriwa kwenye kiwanda hicho ili kuondoa tofauti za mishahara hali ambayo ijenga motisha kwa wafanyakazi.
Kiwanda cha A to Z kilichopo eneo la Kisongo mkoani Arusha ambacho kinatengeneza vyandarua, nguo na mifuko mbalimbali
ikiwemo ya saruji kimeajiri zaidi ya wafanyakazi 7500 ambapo asilimia 80 ya wafanyakazi wote ni wanawake.

 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza wawekezaji kote nchi walipe kodi za serikali mapema kodi ambazo
zitatumika   kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania itaendelea kujenga na kuimarisha mazingira bora kwa wawekezaji ili kuhakikisha
wawekezaji wanafanyakazi zao vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa na ya wawekezaji.

0 maoni:

Chapisha Maoni