Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akifunua kitambaa
kuashiria
uzinduzi rasmi wa Mradi wa Umeme wa Maji wa Kilowati 430 katika Kata ya
Ikondo
mkoani Njombe. Wengine katika picha ni
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Rehema Nchimbi (wa kwanza kushoto), Mbunge wa
Lupembe, Joram Hongoli (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya
(EU), Jane Nunes
(wa Tatu kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
Dkt
Gideon Kaunda (wa pili kulia) na Balozi wa Italia nchini, Roberto
Mengoni (wa
Nne kulia).
............................................
Na Teresia
Mhagama
Naibu Waziri
wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amezindua mradi wa umeme wa Kilowati
430 unaotokana na maporomoko ya maji katika Kata ya Ikondo mkoani Njombe ambapo
mpaka sasa zaidi ya wateja 1140 wameunganishiwa umeme huku zoezi hilo likiwa ni
endelevu.
Uzinduzi huo
uliofanyika katika Kata hiyo ulihudhuriwa na Balozi wa Italia nchini
Tanzania, Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa
wilaya ya Njombe, wananchi wa Kata ya Ikondo, Shirika lililotekeleza mradi huo
la CEFA, watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) na Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO).
Dkt. Kalemani
alisema kuwa mradi huo umetekelezwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya
CEFA kutoka Italia na kugharamiwa kwa pamoja kati
ya Jumuiya ya Ulaya na Serikali ya Tanzania kwa jumla ya Dola za Marekani
110,209.
Aliongeza kuwa
mradi huo wa umeme utasambazwa katika vijiji vilivyoko kata za Ikondo, Matembwe
na Lupembe na ziada itakayobaki inaingizwa kwenye gridi ya Taifa.
" Habari
njema ni kuwa tayari vijiji Saba vimeunganishiwa umeme kupitia mradi huu, hii
inatimiza moja ya malengo ya Serikali ya kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji
wa nishati bora katika maeneo ya vijijini kupitia asasi za kiraia,"
alisema Dkt. Kalemani.
Alisema kuwa,
hadi kufikia mwezi Juni, 2016 idadi ya wananchi wanaopata huduma ya umeme
imefikia asilimia 40 huku vijijini ikiwa ni asilimia 24 na kueleza
kuwa juhudi zaidi zinafanyika ili kufikia lengo la kuunganisha umeme kwa
asilimia 75 ya wananchi ifikapo mwaka 2025.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni