WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameongoza mamia ya wabunge, viongozi wa kitaifa na
watumishi wa Ofisi ya Bunge kuuaga mwili wa Spika Mstaafu, Samwel
Sitta.
Bw.
Sitta alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 7 katika hospitali ya
Technical University of Munich nchini Ujerumani.Akizungumza wakati wa
kuuaga mwili huo Bungeni mjini Dodoma leo (Ijumaa, Novemba 11, 2016),
Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, mke
wa marehemu Mheshimiwa Magreth Sitta, mama wa marehemu Hajat Zuena
Fundikila na familia ya marehemu na wabunge wote.
“Nitumie
fursa hii pia kukupa pole Mheshimiwa Spika kwa pigo ambalo Bunge lako
tukufu imelipata kwa kumpoteza mmoja wa viongozi mahiri wa Bunge hili
katika historia ya nchi yetu. Msiba uliotupata wa
Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa (2005-2010) na Mbunge Mstaafu wa jimbo la
Urambo mkoani Tabora ni mzito.”
Amesema
Bw. Sitta alikuwa mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na
maendeleo. “Serikali imepokea taarifa za msiba huu kwa mshtuko mkubwa.
Historia ya Mzee Sitta ni pana sana. Tunatambua utumishi uliotukuka
katika nyadhifa mbalimbali alizozitumikia. Tutamkumbuka kwa utumishi
wake,” amesema.
Waziri
Mkuu ameongeza kuwa: “Tuzidi kumuomba Mwenyezi Mungu kila mtu kwa imani
yake ili tuweze kufikia japo mema machache aliyoyatenda katika enzi za
uhai wake.”
Enzi
za uhai wake Mhe. Sitta alibahatika kufanya kazi na Marais wa awamu nne
zilizopita tangu ya kwanza ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere, akiwa mbunge kwa miaka 30.
Nyadhifa
nyingine alizowahi kushika ni pamoja na Mkuu wa Mikoa ya Iringa na
Kilimanjaro, Waziri wa Ujenzi, Waziri anayesimamia Ustawishaji Makao
Makuu, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Afrika Mashariki na
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.
Mke wa
Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (wapili kulia) akimfariji mjane wa
Spika Mstaafu Mama Margareth Sitta baada ya mwili wa Spika Mstaafu,
Marehemu Samuel Sita kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba
11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji mjane wa Spika Mstaafu Mama Margareth
Sitta baada ya mwili wa Spika Mstaafu, Marehemu Samuel Sita kuwasili
kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai pamoja na viongozi
wengine wakiusubiri mwili wa Spika mstaafu, Samuel Sitta uteremshwe
kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016
Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta ukiteremshwa kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016.
Mwili wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta ukiingizwa bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwili wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta ukiingizwa bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwili wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta ukiingizwa bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao maalum cha bunge cha
kumuenzi Spika Mstaafu, Samuel Sitta, bungeni mjini Dodoma Novemba 11,
2016.
Waziri Mkuu Mstaafu, Samuel Malecela akimpa pole mjane wa Spika Mstaafu, Margareth Sitta bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016.
1A2358
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye jeneza la
Spika Mstaafu Samwel Sitta, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Spika Mstaafu,
Samuel Sitta, bungeni mjini Dodoma, Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
0 maoni:
Chapisha Maoni