Posted by Esta Malibiche on Nov 15,2016 in NEWS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania Dk. Serafina Mkuwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha
jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim kwenye moja ya mabanda yaliokuwa yanatoa huduma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa uzazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Sehemu ya Wanawake waliojitokeza kwennye uzinduzi huo.
………………………………..

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amewahakikishia wananchi kuwa serikali imeweka mipango na mikakati
thabiti ya kukabiliana na idadi kubwa ya vifo vinasababishwa na saratani
hasa saratani ya matiti na mlango wa kizazi kote
nchini.
nchini.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika viwanja vya
furahisha jijini Mwanza wakati akizundua kampeni ya uchunguzi wa
saratani ya matiti na mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa
kizazi mkoani humo.
Katika
hotuba yake kwa mamia ya wananchi wa mkoa wa Mwanza waliojitokeza
katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania
ikiwa ni nchi mojawapo Kusini mwa Jangwa la Sahara ina kiwango cha juu
cha vifo vya saratani ya matiti na mlango wa kizazi ambapo asilimia 60
ya vifo vyote vinavyotokea Kusini mwa jangwa la Sahara vinasababishwa
na saratani hiyo.
Makamu
wa Rais amesema kuwa vifo vingi vinatokana na uelewa mdogo, imani
potofu,gharama kubwa za matibabu,unyanyapaa na kuwepo kwa vituo vichache
wa kufanyia uchunguzi hapa nchini ambapo kwa sasa tiba ya mionzi
inapatikana katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Roas, Dar es Salaam.
Katika
kukabiliana na tatizo hilo, Makamu wa Rais amesema kuwa Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imepokea kiasi cha
shilingi bilioni Tano kutoka Benki ya Dunia fedha ambazo zitawezesha
vituo Vitatu kwa kila Halmashauri ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za
uchunguzi na matibabu ya mapema ili wanawake kote nchini hasa wale wale
wa vijijini waweze kupata huduma hizo kwa urahisi na kwa ukaribu kwenye
maeneo wanayoishi.
“Wote
ni mashuhuda kwa namna saratani ya mlango wa kizazi inavyosababisha
vifo vingi hali ambayo hutokana na magonjwa wanaogundulika na ugonjwa
kuwa tayari wamefikia hatua isiyotibika na kwa pamoja saratani hizi
mbili husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akinamama”
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa kwa sasa tayari kuna vituo takribani 300
vinavyotoa huduma za upimaji wa dalili za awali katika vituo vya afya
kote nchini na hivyo vituo vipya vitaongeza huduma endelevu ili
kupunguza vifo vitokanavyo na saratani.
Makamu
wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wanaume kote nchi kuunga mkono
kampeni hiyo kwa kuwaruhusu wanawake na wasichana kwenda kupima saratani
hiyo na amewapongeza na kuwashukuru wanaume wa mkoa wa Mwanza kwa
kuwasindika wake zao na watoto wao wa kike kwenda kwenye vituo vya afya
kwa ajili ya kupima saratani hiyo na kupatiwa tiba.
Makamu
wa Rais amepongeza Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania- MEWATA na
wadau wote kwa kuanda zoezi la huduma za uchunguzi wa dalili za awali za
saratani ya mlango wa kizazi. Kwa upande wake, Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Tanzania ni
miongoni mwa nchi zenye wagonjwa wengi wa saratani ya mlango wa kizazi
na pia ndiyo
inaongoza katika nchi za Afrika mashariki.
inaongoza katika nchi za Afrika mashariki.
Amesema kuwa idadi ya wanawake 6241 hugundulika kuwa na saratani kila mwaka na kati yao zaidi ya nusu yaani 4355 hufariki dunia.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
0 maoni:
Chapisha Maoni