Posted by Esta Malibiche on Nov 20,2016 in NEWS
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Pwani, Mh. Subira Mgalu
ametembelea Zahanati ya Viziwaziwa Jimbo la Kibaha Mjini ambayo
ilikuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa madaktari, wauguzi pamoja
na nyumba za watumishi wa Afya ambapo ameweza kuchangia fedha za ukarabati wa
nyumba moja wapo ili watumishi hao warejee kwenye nyumba hizo.
Akiwa katika ziara hiyo, alieleza kuwa, Zahanati hiyo inachangamoto ya
Madkatari na Wauguzi kutokaa kwenye Nyumba zilizojengwa kwa ajili yao na hivyo
kuleta Usumbufu Mkubwa Kwa Wananchi wanapohitaji Huduma za Matibabu ya Dharura
nyakati za Usiku hasa akina Mama Wajawazito pamoja na kuweza kusikiliza hoja
zao ilikujua tatizo nini na kuzitatua.
Katika ziara yake hiyo, Mh. Subira Mgalu ameweza kufanya ukaguzi
wa Zahanati na Nyumba za waganga na kisha kushiriki katika kutatua changamoto
alizokutana nazo katika Zahanati hiyo huku akichangia kiasi cha shilingi Laki
tatu taslimu alizomkabidhi Diwani wa Kata hiyo.
“Nimekuta changamoto nyingi ikiwemo watumishi wa Zahanati
hiyo kukimbia nyumba ambayo haikuwa na
maji. Nimechangia kiasi cha Laki Tatu katika gharama zinazotakiwa kuunganisha
Maji kwenye Zahanati na nyumba hizo, Wananchi watachimba mtaro ili kuwafanya
Madktari wetu warejee kwenye Nyumba hizo zilizokosa maji.” Alieleza Mh. Subira
Mgalu.
Hata hivyo, Mhe. Subira Mgalu amekemea Imani za Kishirikina
zinazokuwa sababu ya Watoa Huduma za Afya kuzikimbia Nyumba hizo ambapo
amewaomba Wazee wa Viziwaziwa warekebishe
mazingira kama yapo vibaya huku akiwaomba Madktari na Wauguzi wasiamini mambo
ya Kishirikina kwani Serikali haimini ushirikina.
Katika ziara hiyo, pia Mhe. Subira Mgalu aliambatana na
Waheshimiwa Madiwani akiwemo wa Viti
Maalum , Diwani wa Kata ambapo walisaidiana nao kujibu kero za Wananchi.
Na .Esta Malibiche
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Pwani, Mh. Subira Mgalu akiongozwa katika kukagua moja ya maeneo ya Zahanati ya Viziwaziwa |
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Pwani, Mhe. Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Viziwaziwa Kibaha wakati wa ziara yake hiyo ya kutatua changamotombalimbali. |
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Pwani, Mh. Subira Mgalua akipokea taarifa ya Zahanati ya Viziwaziwa. |
Mkutano huo ukiendela, Wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Pwani, Mh. Subira Mgalu. |
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Pwani, Mh. Subira Mgalu akisisitiza jambo katika mkutano huo likiwemo Wazee wa Viziwaziwa kurekebisha kasoro zilizopo. |
0 maoni:
Chapisha Maoni