Posted by Esta Malibiche on Nov 29,2016 in TEKNOLOJIA
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Inj. Gerson Lwenge akiangalia aina ya bomba lililotumika kwenye mradi wa
Ruvu Chini na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited,
Nicolas Loh (kulia) pamoja na Meneja Biashara, Ryan Koh.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiwa kwenye karakana ya kiwanda hicho.
Mafundi wakiwa kazini katika karakana ya Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Inj. Gerson Lwenge akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanzania Steel
Pipes Limited, Nicolas Loh na kujionea moja ya mabomba yanayotengenezwa
na kiwanda hicho.
……………………………………………………..
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Inj. Gerson Lwenge mwishoni mwa wiki alitembelea Kiwanda cha Tanzania
Steel Pipes Limited (TSP) kilichopo Shekilango, Dar es Salaam.
Kiwanda hicho kinachotengeneza
mabomba ya maji, ambayo pia yanatumika katika utekelezaji wa miradi ya
maji nchini, ukiwemo mradi ya maji ya Ruvu Chini, KASHWASA na Ruvuma.
“Nimeridhishwa na uwekezaji wa
kiwanda hiki cha mabomba, ambacho kina uwezo wa kuzalisha mabomba yenye
ubora wa kutekeleza miradi yetu ya maji nchini”.
“Hii ni hatua kubwa kwa nchi yetu
ikizingatiwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuinua uchumi
wa viwanda nchini, hivyo maendeleo ya kiwanda hiki ni hatua nzuri ya
kufikia lengo hilo”, alisema Waziri Lwenge.
Inj. Lwenge alisema uwezo ilionao
kiwanda hiki ni chachu ya maendeleo kwa Sekta ya Maji na Umwagiliaji
kwani kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikununua mabomba kutoka nje ya
nchi, na hata yanayotengenezwa hapa mengi ni ya plastiki ambayo hayadumu
muda mrefu ukilinganisha na ya chuma.
Naye Mkurugenzi wa kiwanda cha
Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited (TSP) alisema nia yao kubwa ni
kutengeneza bidhaa nzuri zenye ubora wa kimataifa na kushindana katika
soko la kimataifa, na kuiomba Serikali itumie bidhaa za wawekezaji wa
ndani zenye ubora wa hali ya juu.
Alisisitiza bidhaa zao
zinatengenezwa hapa nchini tangu hatua ya awali na wala si kuagizwa
kutoka nje, zina uwezo wa kudumu mpaka miaka 50, zinatumika nje ya nchi
ikiwemo Rwanda, ambapo zinatumika kwenye miradi mikubwa ya maji.
Dhumuni la ziara hiyo lilikuwa ni kujionea uwezo wa kiwanda hicho kwa upande wa uzalishaji na ubora wa bidhaa zao.
0 maoni:
Chapisha Maoni