Jumatano, 9 Novemba 2016

Ujumbe wa Rais Magufuli baada ya Donald Trump kushinda uchaguzi wa Marekani


Muda mchache baada ya Donald Trump kuibuka mshindi wa uchaguzi mkuu wa Marekani, taarifa za ushindi huo zimemfikia na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Magufuli ameandika ujumbe wa kumpongeza Donald Trump kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani na matumaini yake ni kuwa urafiki wa Tanzania na Marekani utaendelea.
“Hongera kwa Rais mteule na kwa watu wa Marekani kwa kufanya uchaguzi wa kidemokrasia, Ninawahakikishia kwa watu wa Tanzania tutaendeleza urafiki”

0 maoni:

Chapisha Maoni