Jumatano, 23 Novemba 2016

RC MBEYA -JITIHADA ZA PAMOJA ZINAHITAJIKA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA UKIMWI



Posted by Esta Malibiche on Nov 23,2016 in NEWS


Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla  amewaomba viongozi, watendaji na wananchi wote kwa pamoja kuongeza kampeni za kudhibiti maambukizi ya ukimwi ili kufikia malengo ya kuwa na jamii yenye nguvu kazi ya uhakika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa   amewasihi wananchi kupima Afya zao.
 

Hayo ameyasema Leo katika ufunguzi wa Mafunzo ya udhibiti wa ukimwi kwa mikoa ya nyanda za juu kusini yaliyooandaliwa na TACAIDA  kwa kushirikiana WALTER REED PROGRAM ya ubalozi wa marekani na Henry Foundation.

‘’’’Watanzania wa rika zote, na viongozi wa ngazi zote tuungane katika uhamasishaji wa upimaji Afya na kudhibiti ukimwi. Bila jamii yenye Afya hakuna viwanda, hakuna kilimo na uchumi utayumba’’’AlisemaMakalla.
Makalla alisema Mikoa ya nyanda za juu kusini ina kiwango cha juu cha maambukizi,ambapo Mkoa wa Mbeya ni 9%,Ruvuma 7%,Rukwa 6.2% na Katavi 5.9%, Kiwango cha maambukizi VVU kitaifa ni 5.1%.
‘’’’Bila kuwa na jamii yenye Afya njema hatutafikia malengo vya kuwa na viwanda, kilimo na uchumi mzuri kwani wanaoathirika zaidi ni Vijana ambao ndiyo nguvu kazi kubwa ya Taifa’’’’’Alisema Makalla.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya udhibiti wa ukimwi kwa mikoa ya nyanda za juu kusini yaliyofanyika Mkoani Mbeya.




0 maoni:

Chapisha Maoni